Ili kuendelea kuwahakikishia usalama Watoto chini ya umri wa miaka mitano, Serikali imekuja na kampeni ya awamu ya nne ya Chanjo ya Polio ambapo watoto 14,690,597 watapatiwa chanjo hiyo.
Kampeni hiyo inatarajiwa kuanza December 1 hadi 4, 2022 na itafanyika nchi nzima , Polio ikiwa ni miongoni mwa magonjwa hatarishi zaidi kwa watoto ambapo virusi vya polio huvamia mfumo wa Neva na madhara yake husababisha kupooza au hata Kifo.
Hayo yamebainishwa na afisa Program ya Chanjo Bi. Lotalis Gadau Leo Novemba 30, 2022 wakati wa Utoaji Semina elekezi kwa Wanahabari jijini Dodoma inayogusa kutoa elimu kuelekea katika kampeni ya polio ambapo amesema kampeni hiyo itakuwa ni nyumba kwa nyumba.
"Kwa utoaji wa chanjo za matone ya Polio ikilenga Watoto kuanzia Umri chini ya Miaka mitano sambamba na Timu za wachanjaji ambapo kutakuwepo na waangalizi wa kujitegemea katika Kila Mkoa nchini ili kukamilisha zoezi hilo,"Bi.Lotalis
Ametaja njia za maambukizi ya ugonjwa huo sambamba na dalili ikiwa ni pamoja na homa, uchovu, maumivu, ya kichwa, kutapika, kukakamaa shingo na maumivu ya Viungo.
“Ugonjwa huu huambukizwa kwa kuingia mwilini kwa njia ya mdomo, kunywa Maji,au chakula ambacho kimechafuliwa na kinyesi kutoka kwa Mtu aliyeambukizwa virusi hivyo na virusi huongezeka ndani ya utumbo na hutolewa na mtu aliyeambukizwa kwenye kinyesi, ambacho kinaweza kupitisha virusi kwa wengine”
Aidha ameeleza Hali ilivyo kwa sasa juu ya ugonjwa wa Polio katika maeneo mbalimbali ndani ya Bara la Afrika.
“Zambia tayari kuna kisa kimoja, wenyewe wanajiandaa na awamu ya Tatu, na kwetu Tanzania tunamshukuru mungu bado kisa ni kile kile hatujapata kingine, lakini bado hakijalemaa, bado tunaendelea na ufuatiliaji kwa kuchukua Sampuli kuhakikisha kwamba tunapeleka maabara mwisho wa siku watoto wetu wawe salama.DRC CONGO bado kuna vimlipuko vya hapa na pale lakini ambao tulienda nao sambamba tokea tunaanza mwanzo ni Malawi, Msumbiji, Zimababwe na Zambia”
Pia ameeleza mikakati inayotumika katika kuhakikisha wanatokomeza ugonjwa huo hapa nchini ikiwa ni pamoja na kufanya kampeni za kutoa elimu itakayoambatana na utoaji wa Chanjo.
“Tunachojitahidi ni kuonyesha kwamba tunaimarisha utoaji wa chanjo za kila siku kuhakikisha kwamba watoto wetu wanakamilisha Ratiba zao za chanjo ili endapo hata Kirusi kikija kikimkuta mtoto ameshapata kinga kamili kinakuwa hakina nafasi na kwa awamu hii tunalenga kuwafikia watoto wapatao Millioni 14 laki sita na Tisini, Mia tano Tisini na Saba kwa awamu hii ya nne”
Amehitimisha kwa kusema kuwa zoezi hili litafanyika kwa kupita nyumba kwa nyumba na kisha nyumba ambayo itakuwa imepata chanjo itawekwa alama ya Tiki ili kuonesha tayari imekwisha kupata huduma ili kurahisisha utekelezaji wa zoezi hilo na kuepusha usumbufu wa foleni na upotevu wa muda.
No comments:
Post a Comment