Tanzania Mwenyeji Tamasha la Muziki Afrika - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, November 4, 2022

Tanzania Mwenyeji Tamasha la Muziki Afrika


Baada ya kuratibu kwa mafanikio Mashindano ya Dunia ya Urembo, Utanashati na Mitindo kwa Viziwi Duniani, mtu anaweza kusema #NiTanzaniaTena.

Novemba 24-26 mwaka huu wataalamu na wadau wa muziki Barani Afrika wanakutana Tanzania kwa siku tatu za watu kubadilishana mawazo na maonesho ya muziki wa Afrika na jiji la Dar es Salaam tena katika kumbi za Julius Nyerere (kwa mkutano) na BreakPoint Makumbusho (kwa maonesho ya muziki jioni) linakwenda kuwa mwenyeji wa tano tangu mkutano huo mkubwa uanze kufanyika Afrika.

“Ni fursa kwa wasanii wa Tanzania kukutana na wadau wa kubwa wa muziki Afrika kama wasanii wenzao, wauzaji kazi za muziki kama Sony, Boomplay na Universal na kwa ujumla ni fursa ya kukua,” alisema Eddie Hatitye Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Access ya Afrika Kusini inayoratibu mkutano huo kwa kushirikiana na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ya Tanzania.

“Mi naona mkutano huu unakuja kujibu maswali yetu yote kuhusu vipi tunaupeleka mbele muziki wetu tunakutana vipi na wadau wakubwa Afrika na duniani. Shirikisho la muziki linawaomba wadau wote tujisajili maana ndio sharti la kuhudhuria mkutano huu katika pages za Access kwani ni bure kabisa,” alisema Msanii Fid Q, Katibu wa Shirikisho la Muziki Tanzania.

“Ni TanzaniaTena; Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia jambo hili kubwa Afrika na linalowaleta wadau kutoka Afrika na kote duniani, imedhamini sehemu ya mkutano huu kwa nia ya kuwaletea karibu wasanii wetu fursa za kujua masoko makubwa zaidi na fursa za kujuana. na wakubwa zaidi. Sisi tumetimiza wajibu wetu,” alisema Dkt. Hassan Abbasi, Katibu Mkuu Wizara ya Sanaa katika mkutano wa maandalizi ya shughuli hiyo na wanahabari uliofanyika leo Ijumaa, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment