WAANDISHI WA HABARI JIJINI DODOMA WAPIGWA MSASA JUU YA MPANGO WA BIMA YA AFYA KWA WOTE. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, November 9, 2022

WAANDISHI WA HABARI JIJINI DODOMA WAPIGWA MSASA JUU YA MPANGO WA BIMA YA AFYA KWA WOTE.

Afisa Mawasiliano kutoka Wizara ya Afya Saidi Makora ,akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo pichani) leo Novemba 09,2022 jijini Dodoma katika semina ya kuwajengea uelewa juu ya mpango wa Bima ya Afya kwa wote.
Afisa Mawasiliano kutoka Wizara ya Afya Saidi Makora ,akizungumza na waandishi wa habari  leo Novemba 09,2022 jijini Dodoma katika semina ya kuwajengea uelewa juu ya mpango wa Bima ya Afya kwa wote.

Na Okuly Julius-Dodoma

Waandishi wa Habari Jijini Dodoma wametakiwa kutumia kalamu zao vizuri kuelimisha wananchi juu ya kujiunga na mpango wa Bima ya Afya kwa Wote ili kujenga jamii yenye afya bora kwa maslahi ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza katika mafunzo maalumu ya kuwajengea uelewa waandishi wa habari leo Novemba 09,2022 Jijini Dodoma, juu  ya umuhimu wa bima ya afya kwa wote nchini,Afisa Mawasiliano kutoka Wizara ya Afya Saidi Makora, amesema kuwa dhumuni kubwa la Serikali ni kuweka mfumo mzuri wa watu kupata huduma stahiki ya afya bila kutumia gharama kubwa.

Aidha,Makora amesema lengo lingine ni kupanua wigo mpana wa upatikanaji wa huduma ya Afya kwa wote na mahali popote na kupunguza gharama kubwa za matibabu ambazo zimekuwa zikitumika katika malipo ya kupata huduma ya hiyo.

Hatahivyo ameongeza kuwa katika kuhakikisha Bima ya Afya kwa Wote inatumiwa na Watanzania wote,serikali imefungamanisha huduma hiyo na huduma nyingine za kijamii kama Hati za kusafiria,kitambulisho cha Taifa,usajili wa laini za simu nk,lengo likiwa ni kuongeza msukumo wa wananchi kupata huduma ya Afya kwa urahisi.

"Tumeona ni vyema kufungamanisha Bima ya Afya kwa Wote na huduma nyingine za Kijamii ikiwepo leseni za udereva,kitambulisho cha taifa,Hati ya kusafiria mnajua ni kwa nini? Ili kila mmoja aone uzito na umuhimu wa kujiunga na Bima ya afya kwa wote hiyo nadhani itaongeza msukumo mkubwa kwa wananchi kupata huduma ya Afya kwa urahisi na ufanisi," Amesema Makora

Ikumbukwe kuwa serikali inaendelea kuratibu maandalizi ya sheria ya bima ya Afya kwa wote ya mwaka 2022 ambapo muswada wa sheria hiyo umesomwa kwa mara ya kwanza Bungeni sept 23,2022 na Unatarajiwa kusomwa kwa mara ya pili na ya tatu Ijumaa ya wiki hii Nov.11 ,2022 lengo la sheria hiyo inayopendekezwa likiwa ni kuwezesha wananchi kupata huduma bora za Afya bila kikwazo cha fedha.

No comments:

Post a Comment