Maafisa wanasema watu 34 walikufa kote Marekani, huku eneo lililoathirika zaidi likiwa ni jiji la Buffalo, katika jimbo la New York.
Vifo vinne viliripotiwa Canada wakati basi lilipobingiria kwenye barabara yenye barafu karibu na mji wa Merritt, katika jimbo la magharibi la British Columbia.
Kiwango hiki cha dhoruba ya msimu wa baridi hakijawahi kushuhudiwa,kuanzia Canada kusini hadi Rio Grande.
Watabiri wanasema dhoruba itapungua katika siku chache zijazo lakini ushauri umetolewa kuzuia watu kusafiri isipokuwa kwa hali ya dharura.
Dhoruba hiyo imesababisha maafa kwa siku kadhaa lakini huduma ya umeme umerejeshwa baada ya kukatika hapo awali.
Chini ya wateja 200,000 hawakuwa na nishati kufikia Jumapili alasiri. Shirika la Habari la Associated linaripoti.
Maelfu ya safari za ndege zimekatishwa, na kuzuia watu wengi kufikia familia zao wakati wa Krismasi.
CHANZO NI BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment