"Magari ya angani yasiyo na rubani" yalikiuka anga ya Korea Kusini katika maeneo ya mpakani karibu na mkoa wa Gyeonggi, walisema wakuu wa jeshi la nchi hiyo.
Moja ya ndege zisizo na rubani ziliruka hadi mji mkuu Seoul, kulingana na ripoti.
Jeshi la Korea Kusini lilisema kuwa lilifyatua risasi za onyo kabla ya kutuma ndege na helikopta kuziangusha droni hizo
Moja ya ndege za kivita, ndege nyepesi ya KA-1, ilianguka baadaye, lakini marubani wake wawili walinusurika bila kujeruhiwa.
Ndege hiyo ilianguka chini katika Kaunti ya Hoengseong, mashariki mwa Seoul, mara baada ya kupaa kutoka kituo cha anga katika mji wa karibu wa Wonju, kulingana na jeshi la wanahewa, lililonukuliwa na shirika la habari la Yonhap.
Korea Kusini pia ilisimamisha ndege kupaa na kutua katika viwanja vyake vya Incheon na Gimpo kwa takriban saa moja.
Mara ya mwisho ndege isiyo na rubani ya Korea Kaskazini kuvuka mpaka ilikuwa miaka mitano iliyopita mnamo Juni 2017.
CHANZO NI BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment