Na Mwandishi wetu Dar-es-salaam
Mwandishi na Mtangazaji wa MVIWATA FM, inayosimamiwa na Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania MVIWATA mkoani Morogoro, Shua Ndereka ni miongoni mwa waandishi 12 waliotunukiwa tuzo za Umahiri wa Uandishi wa habari za watoto nchini.
Shua ametunukiwa tuzo ya mfano kwa kujitolea katika Uandishi wa habari za watoto, akipewa ngao (trophy) cheti na fedha taslimu.
Hii ni mara ya pili Kwa mwandishi huyo kupata tuzo. Mwaka 2021 alitambuliwa kwa kupewa cheti cha uandishi bora wa habari za watoto.
Ndereka pamoja na washindi wengine kutoka vyombo mbalimbali vya habari, walikabidhiwa tuzo hizo Dec 29, 2022 jijini Dar es Salaam.
Washindi wengine ni Faraja Masinde, Stanslaus Lambati, Anold Kailembo, Vicky Kimaro, Sabina Martin, Aidan Mhando, Tumaini Msowoya, Anna Sombida na Marko Maduhu.
Hafla ya tuzo hizo iliandaliwa na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kwa kushirikiana na Ofisi ya Tanzania ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kudumia watoto (UNICEF Tanzania).
Tuzo hizo ni sehemu ya utekekezaji wa mradi wa undishi wa habari za watoto unaoratibiwa na TEF chini ya ufadhili wa UNICEF ulioanza tangu mwaka 2017.
Hii ni mara ya nne kwa TEF na UNICEF kuwatambua Waandishi waliofanya vizuri katika kupaza sauti za watoto kupitia vyombo mbalimbali vya habari nchini, wakitangaza taarifa zinazolenga kushawishi mabadiliko ya kisera na kisheria yanayowagusa watoto.
No comments:
Post a Comment