Na Mwandishi wetu Arusha
Aidha imesititiza kuwa ziara za nje anazofanya Rais Dk, Samia zinaleta tija zaidi kwani akirudi nchini harudi bure na zinafungua milango nje na ndani ya nchi.
Akiongea na vyombo vya habari jijini Arusha,mwenyekiti wa jumuiya hiyo Taifa ,Fadhili Maganya amesema kuwa wanampongeza Rais Dk,Samia Suluhu Hasan kwa kuruhusu kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa nchini kikidai itachochea maendeleo kwa taifa.
Amesema, Rais alisema mikutano ya vyama vya siasa itumike kukosoa bila kugombana ikiwemo kuanza kukwamua mchakato wa katiba.
Maganya ameongeza kuwa Rais ameridhia kuendelea kuangalia sheria mbalimbali kwaajili ya kuziboresha kwa maslahi mapana ya nchi na kuahidi ushirikishwaji wa wadau na makundi mbalimbali katika kuziboresha sheria hizo
"Tunatoa wito kwa watanzania wote kumtia moyo Rais Samia kwani umoja na mshikamano ndio msingi wa maendeleo katika nchi yetu" amesema Maganya
Akitoa rai kwa vyama vya siasa kuzingatia sheria,kanuni na miongozo mbalimbali katika utekelezaji wa shughuli za kisiasa hapa nchini ikiwemo kumuunga mkono Rais Samia kwa kuendeleza siasa za maridhiano kwa maslahi mapana na kwa mustakabali wa nchi.
Akizungumzia kuhusu safari anazozifanya Rais Samia nje ya nchi,Maganya ametumia methali ambazo ni mgaa,gaa na upwa hali wali mkavu na kusema kuwa mwenda bure si sawa na mkaa bure ,hivyo Rais anaposafiri kuna fursa mbalimbali anafungua.
Kuhusu mikopo wanayodai anakopa kopa sana,Maganya amesisitiza kuwa Rais anakopa kwa maslahi ya Taifa na nchi kwa ujumla na mikopo inafanya kazi na kazi zinaonekana.
Naye mwenyekiti wa ccm Mkoa wa Arusha,Steven Zelothe amesema kuwa kuondoa katazo la mikutano ya hadhara ya kisiasa kumeleta faraja ,uzalendo ,ujasiri na uongozi imara na kuweka taifa imara.
Amesema kuwa CCM Mkoa wa Arusha,inaunga mkono kwa dhati kuruhusiwa kwa mikutano ya kisiasa na kutaka mikutano hiyo isiende kuleta mtafaruku na kuvuruka amani ya nchi ambayo tumezoea kuwa nayo.
Hata hivyo Zelothe ameongeza kuwa Chama Cha Mapinduzi hakina hofu na mikutano ya wapinzani ila aliwataka wafanye siasa za kiungwa na ustaarabu ili kuleta tija katika maendeleo ya wananchi.
Naye kada wa CCM,Balozi Daniel Njolaay amesema Rais ameona mbali kuamua kuruhusu mikutano ya kisiasa akidai Italeta changamoto kwa serikali na ushindani wa kisiasa.
Amewataka wanachama wa CCM kuwa kitu kimoja kwa sababu baadhi yao ni tatizo lazima wajisafishe.
"Na sisi ndani ya CCM lazima tuwe kitu kimoja kwani matatizo yapo ndani yetu lazima tujitizame na tujisafishe"
**Kama una taarifa yako na unatamani tuichapishe kwenye OKULY BLOG basi usisite kututumia kupitia OkulyJulius@gmail.com au +255785364965 kwa WhatsApp au Telegram Karibu sana**
No comments:
Post a Comment