HATUA ZILIZOCHUKULIWA NA SERIKALI KUHUSU SHULE ZINAZOFUNDISHA WANAFUNZI TABIA CHAFU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, January 17, 2023

HATUA ZILIZOCHUKULIWA NA SERIKALI KUHUSU SHULE ZINAZOFUNDISHA WANAFUNZI TABIA CHAFU


Na Okuly Julius-Dodoma

Serikali imeanza kuchukua hatua kufuatia ripoti iliyochapishwa kwenye vyombo vya habari juu ya uwepo wa baadhi ya shule zinayofundisha wanafunzi maadili mabaya.

Kauli hiyo imetolewa na waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma

Prof.Mkenda amebainisha kuwa Wizara hiyo tayari Imeshawaagiza Kamishina wa Elimu,Mwanasheria wa Wizara hiyo ambapo wameanza uchunguzi katika hizo shule zilizotajwa na baada ya hapo watakuja na majibu.

"Hatuwezi kusema kesho au keshokutwa watupatie majibu maana ni suala linalohitaji uchunguza na kupatikane majibu ya usahihi ili tuepuke kuharakisha mambo alafu baadae mambo yakaharibika ndio maana tumemwagiza Kamishina aa elimu mwenyewe sio Mwakilishi na Mwanasheria wa Wizara na sio Mwakilishi tupate majibu yaliyokamilika,"amesema Prof.Mkenda 


Aidha waziri Mkenda ameongeza kuwa wizara imekusudia kuchukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa namba maalumu kwaajili ya kutoa taarifa ya vitendo hivyo katika shule za umma au binafsi.

"Katibu Mkuu atatoa namba maalum kwa ajili ya kila mmoja kupiga simu pale ambapo atabaini kuna vitendo hivyo vichafu shuleni,"amesema Prof.Mkenda 

Pamoja na hayo Prof.Mkenda amesema kuwa Serikali itahakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa kwani vitaondoa uaminifu kwa wazazi juu ya kuwapeleka watoto wao shule.

Kwa upande mwingine Prof.Mkenda amesema kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itashirikiana na Wizara zingine za kisekta kupata ufumbuzi na kukomesha matukio kama hayo.




No comments:

Post a Comment