KANISA LAWAVIKA MAVAZI YA SHULE WATOTO 60 BIGWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, January 17, 2023

KANISA LAWAVIKA MAVAZI YA SHULE WATOTO 60 BIGWA


Na Shua Ndereka- Morogoro

Watoto 60 kutoka mtaa wa Bigwa Sokoni kata ya Kilakala, Manispaa ya Morogoro wamepokea msaada wa sare za shule na vifaa vya kusoma na kujifunzia ili kupata elimu bora baada ya kujiunga na Elimu ya Msingi Mwaka 2023.

Msaada huo umetolewa na Kanisa la Christian worship Center linaloongozwa na Mchungaji kiongozi Venance Gasper, baada ya Mwenyekiti wa mtaa huo Justine Mkoba kuomba ufadhili kwa watoto hao ili kusaidia familia zisizo na uwezo wa kugharamia mahitaji maalumu ya shule.

Akielezea mafaniko katika kipindi cha Uongozi wake katika Mkutano wa Mtaa uliofanyika Januari mwaka huu, Mwenyekiti wa Mtaa wa Bigwa Sokoni Justine Mkoba alisema, watoto hao wapo wanaoishi katika mazingira magumu na baada ya kuona uhitaji mkubwa katika Mtaa wake ndipo alipomfuata Mchungaji Venance Gasper kumueleza ili kuwasaidia watoto hao kisha akakubali.

"Hawa watoto wako 60 ni wananchi wangu, wengine wanaishi katika mazingira magumu nilimfata Mchunguaji kiongozi wa kanisa la Christian worship Center Venance Gasper kwa sababu huwa wanatoa msaada kwa watoto na mimi nikamwambia asaidie watoto wa Mtaa wangu, alinikubalia na kuagiza niwaite watoto na wazazi wao kisha akaja kuwaona, na sasa leo wanapata madaftari, penseli, vifutio na Sare za Shule".


Naye Mchunguaji kiongozi wa Kanisa la Christian worship Center Venance Gasper alisema Kanisa limekua na utaratibu wa kuwawezesha wanafunzi kama sehemu ya kusaidiana na jamii pamoja na Serikali kuondoa vikwazo na changamoto za Mtoto kupata Elimu.

"Sisi kama Kanisa tumeona tuisaidie Serikali na kwa sadaka yetu hii tunatoa mchango kwa Mtaa wa Bigwa Sokoni ili wapate elimu na hao watoto tutakwenda nao hadi darasa Sita, lengo letu ni kuona watoto hawa wanafika Chuo kikuu".

Aidha Mgeni Rasmi katika Mkutano huo alijuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Morogoro Women Voice and Connection inayojihusisha na kuwainua wanawake kiuchumi, Tekra Mbiki wakati akitoa hotuba yake, aliahidi kuwanunuliwa watoto hao Masweta ya Shule.

"Na sisi kama wananchi na Taasisi ya wanawake Mwenyekiti amesema tuwapokee watoto, tunaahidi kutoa masweta kwa watoto wote 60 kwa sababu kila Mtoto anahaki ya kupata Elimu bora".

Kwa upande wao baadhi ya watoto kutoka mtaa wa bigwa sokoni, wameshukuru uongozi wa mtaa huo, pamoja na wote walioguswa kuwasaidia, kupitia risala iliyosomwa na Neema Justinebele ya mgeni Rasmi. 

"Hakika siku ya leo ni siku ya furaha sana kwetu sisi watoto, kwani tunakabadhiwa mahitaji muhimu ya Shule kwa ajili ya kutuwezesha katika masomo yetu Mwaka huu 2023 na tutapata muda mzuri wa kuhudhuria masomo vizuri pasipo na kisingizio cha kukosa mahitaji ya Shule".

Nao Baadhi ya wazazi waliohudhuria Mkutano huo wamelipokea vyema suala la kusaidia watoto kupata Elimu, akiwemo Yohana Kimenya mkazi wa Mtaa wa Bigwa Sokono alisema misaada hiyo ni mizuri kwa sababu zipo familia ambazo hazina uwezo kwa namna moja mfadhili huyo amewainua watoto katika familia hizo. 

"Nimfurahi Mtoto wangu anakwenda Shule akiwa amependeza ninawashukuru wafadhili hawa, na Mwenyekiti wetu wa mtaa asichoke waendelee kutuangalia sisi wazazi na familia duni ili watoto wote wapate elimu sawa". Alisema Josephine Zenobius.

No comments:

Post a Comment