![]() |
Wahariri wa vyombo vya habari nchini na wadau wa sekta ya kilimo wakisikiliza Hotuba ya Waziri wa Kilimo leo Januari 10,2023 katika ukumbi wa Mabele jijini Dodoma. |
![]() |
Wahariri wa vyombo vya habari nchini na wadau wa sekta ya kilimo wakisikiliza Hotuba ya Waziri wa Kilimo leo Januari 10,2023 katika ukumbi wa Mabele jijini Dodoma. |
Na Okuly Julius-Dodoma
Amebainisha hayo Jijini Dodoma Leo Januari 10,2023 kwenye Mkutano na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari pamoja,watumishi kutoka katika Sekta ya Kilimo pamoja na wadau wengine wa Sekta ya Kilimo hapa nchini.
Bashe amesema kuwa Bajeti ya huduma za Ugani kwa mwaka wa 2022/2023 ni Bilioni 14.5
Pia Mheshimiwa Bashe amesema kuwa katika mwaka wa fedha ujao wa 2023/2024 serikali kupitia Wizara ya Kilimo imedhamiria kujenga mabwawa 110 nchi nzima kwa ajili ya kuendelea kuboresha kilimo cha Umwagiliaji.
Waziri huyo amesema kuwa ifikapo Mwaka wa 2030 Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imejiwekea malengo ya kuhakikisha inajitosheleza kwa mahitaji ya Chakula,inaongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo kupitia kilimo cha umwagiliaji kutoka asilimia 10 iliyopo kwa sasa hadi asilimia 50.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Dkt.Stephan Ngailo amesema kuwa ili kupunguza utegemezi wa kuagiza mbolea kutoka nje ya nchi TFRA inaendelea kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vya ndani vya kuzalisha mbolea.
Ngailo ameongeza kuwa kwa sasa asilimia 90 ya mbolea inayotumika nchini inatoka nje wakati asilimia 10 tu ndio inayozalishwa katika viwanda vya ndani.
"TFRA tunaendelea kuhamasisha uwekezaji wa viwanda vya ndani kuongeza uzalishaji wa mbolea na imani yangu ni kwamba itaongezeka kwani kuna viwanda vimeanza uzalishaji wa mbolea ikiwemo kiwanda cha Intracom na Minjingu ambazo pia zimeanza kuuza Mbolea ,"Amesema Dkt.Ngailo
**Kama una taarifa yako na unatamani tuichapishe kwenye OKULY BLOG basi usisite kututumia kupitia OkulyJulius@gmail.com au +255785364965 kwa WhatsApp au Telegram Karibu sana**
#Okulyblog.blogspot.comUpdates
No comments:
Post a Comment