TANZANIA HAITATUMIA GMO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, January 10, 2023

TANZANIA HAITATUMIA GMO


Na Okuly Julius-Dodoma 

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema, Tanzania haipo tayari kutumia mbegu zilizobadilishwa vinasaba (GMO), lakini itatenga maabara mbili ili kuendelea kujifunza na kuepuka kutumia kitu wasichokijua.

Hayo yamebainishwa leo Jan10, 2023 katika Mkutano unaoendelea ukumbi wa Mabele jijini Dodoma kati ya Waziri huyo, wahariri wa vyombo vya habari pamoja na wadau wa sekta ya kilimo kwa ajili ya kuwaelezea utekelezaji wa Agenda ya 10/30 kilimo biashara.

Aidha amesema wataendeleza tafiti mbalimbali juu ya mbegu zilizobadilishwa vinasaba (GMO) ili kujifunza na kuijua zaidi.

GMO ni mazao yaliyobadilishwa vinasaba, au mazao yaliyoundwa na vinasaba vilivyofanyiwa uhandisi jeni ambapo inatajwa kuwa na athari kwa binadamu, wanyama na mazingira kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment