Na Okuly Julius-Dodoma
Kwani mara nyingi Wakulima wamekuwa wakitumia njia hiyo kuandaa mashamba yao kuelekea msimu wa kilimo jambo ambalo limekuwa likileta athari katika misitu na uoto wa asili.
Waziri Chana ameyasema hayo leo Januari 11,2023, wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza katika zoezi la upandaji Miti katika Bwawa la Swaswa lililopo kata ya Ipagala Jijini Dodoma , Ikiwa ni muendelezo wa upandaji miti kuelekea kilele cha Maadhimisho ya miaka 59 ya mapinduzi ya Zanzibar.
Ambapo Waziri Chana ameongeza kuwa moto huwa una tabia ya kusambaa kulingana na uelekeo wa upepo na kwenda maeneo ambayo hayakukusudiwa kuchomwa hivyo inapelekea uharibifu wa misitu kwani wakulima huchoma moto na kuondoka.
"Wakulima wamekuwa wakitumia njia ya kuchoma moto kuandaa mashamba yao kuelekea msimu wa kilimo jambo ambalo limekuwa likileta athari katika misitu yetu,
Na kuongeza "Tuache kutumia njia hiyo kuandaa mashamba ili kunusuru misitu yetu," amesema Dkt.Chana
Pia amewataka wafugaji kuacha tabia ya kuingiza mifugo katika hifadhi ya misitu na hasa katika miti hiyo inayopandwa kwa sasa kwani mifugo inachochea jangwa na kupelekea athari ambazo zinafika mbali zaidi na kupelekea hata kutokea kwa upungufu wa maji kwani kunakuwepo na uharibifu wa vyanzo vya maji.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Abdallah Mitawi amesema kuwa mapinduzi ya Zanzibar ndiyo Kielelezo cha Muungano,Uhuru na Mshikamano wa Tanzania na imeonekana ni vyema kusherehekea kwa kupanda miti ili kuendelea kukijanisha Dodoma.
Naibu katibu huyo amesema kuwa wamedhamiria kupanda miti zaidi ya elfu 5 ndani ya siku tatu katika Jiji la Dodoma jambo ambalo litaacha kumbukumbu ya kudumu ya miaka 59 ya mapinduzi ya Zanzibar
"Kupanda miti sio kazi ila kazi kubwa ni kutunza miti hii ikue kwani baadhi ya watu hawana desturi ya kutunza miti hivyo niwatake wananchi kutunza miti na kuacha tabia ya kuachia mifugo kula miti waache mara moja," amesema Mitawi
**Kama una taarifa yako na unatamani tuichapishe kwenye OKULY BLOG basi usisite kututumia kupitia OkulyJulius@gmail.com au +255785364965 kwa WhatsApp au Telegram Karibu sana**
No comments:
Post a Comment