Mmiliki wa Mochari Asukumwa Jela Miaka 20 Kwa Kuuza Viungo vya Miili 560 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, January 4, 2023

Mmiliki wa Mochari Asukumwa Jela Miaka 20 Kwa Kuuza Viungo vya Miili 560

Megan Hess(kushoto), akiwasili kwenye Mahakama ya Wayne Aspinall na wakili wake mnamo Jumanne, Januari 3.
Picha: RJ Sangosti. Chanzo: Getty Images


Mmiliki wa zamani wa makafani katika Jimbo la Colorado, Marekani, amehukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani kwa kuwalaghai jamaa za waliofariki na kuuza viungo vya miili ya maiti 560 bila idhini.

Megan Hess, 46, aliungama makosa ya kulaghai zaidi ya familia 200 kwa kupasua na kuuza viungo vya miili ya wapendwa wao ,Hess anaripotiwa kuuza sehemu za miili ya maiti 560 bila idhini ya familia zao Mamake Hess, mwenye umri wa miaka 69, Shirley Koch, pia alikiri kosa la ulaghai na alihukumiwa kifungo cha miaka 15 jela.

Megan Hess, 46, aliungama makosa ya ulaghai mnamo Julai 2022, akiendesha hifadhi ya maiti ya Sunset Mesa. 

              CHANZO NI TUKO.co.ke.


No comments:

Post a Comment