Na Mwandishi wetu
Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wameungana na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) pamoja na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwenye zoezi la kupitia na kuhakiki ufanisi wa dira hizo.
Tarehe 21 Juni mwaka 2022 RUWASA iliingia mkataba na Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), Chuo cha Ufundi Mbeya (MUST) pamoja na Kampuni Tanzu ya COSTECH (DTBi) inayohusu utengenezaji wa dira za maji za malipo kabla ya matumizi (pre paid water meters) na kuzifunga kwenye baadhi ya miradi ya maji kwa majaribio.
Dira hizo zinazotengenezwa na wabunifu wa ndani kutoka taasisi zetu za serikali na wazawa zimefungwa maeneo kadhaa na kuleta ufanisi mkubwa.
Timu inaendelea kujifunza na kutoa maoni yao kwa kila taasisi ili kuboresha maeneo ambayo hayapo vizuri ili dira hizo zilete ufanisi mkubwa kwa mtumiaji na wasimamizi wa miradi ya maji vijijini.
Timu ya wataalamu inapita maeneo ambayo dira hizo zinatengenezwa sambamba na maeneo ambapo dira hizo zimefungwa na kuhakiki ufanisi wake katika utoaji wa huduma
Kwa sasa RUWASA imejidhatiti katika usimamizi wa miradi ya maji vijijini ili iwe endelevu.
No comments:
Post a Comment