SERIKALI YAENDESHA MAFUNZO KWA WAGANGA WA TIBA ASILI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, January 13, 2023

SERIKALI YAENDESHA MAFUNZO KWA WAGANGA WA TIBA ASILI


Na FRED ALFRED-Dodoma

OFISI ya Mkemia Mkuu wa Serikali imeendesha mafunzo kwa waganga wa tiba asili kuhusu mbinu salama na Bora za uandaaji,usindikaji na uchukuaji wa sampuli za dawa asili.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Meneja Maabara Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali John Faustina amesema katika kipindi cha kukabiliana na janga la Uviko -19 duniani, Dawa za tiba asili zilikuwa msaada mkubwa katika kupunguza makali ya maambukizi hayo.


"Ofisi ya Mkemia Mkuu imeamua kutoa mafunzo ya siku tatu ili kuwapa elimu itakayokuwa mwarobaini wa kufumbua changamoto Kwa waganga wa tiba asili ambazo wamekuwa wakikumbana nazo ikiwemo kupoteza kumbukumbu wakati uchanganyaji wa viwatilifu vya tiba,"amesema

Kwa upande upande wake Katibu wa Chama cha Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba asili na Mbadala Lukas Mlipu ameipongeza serikali kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo yatasaidia waganga wa tiba asili kufanya kazi Kwa uhakika.

Alisema baada ya mafunzo hayo kuisha waganga watakuwa wameelika katika nyanja mbalimbali.


"Tunaipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kututambua pia na uongozi wa wilaya ya Kongwa Kwa kutoa ekari 100 kwa ajili ya kupanda miti mbalimbali ambayo itatumika kama dawa hii ni heshima kubwa na tutaendelea kufanya kazi kwa weledi,"amesisitiza.

Mlipu ametaja moja ya changamoto inowakabili ni suala la watu wanaotumia mgongo wa tiba asili kutapeli watu jambo mabalo limesababisha kuwa na sura mbaya kwa jamii.

Mafunzo hayo yatafanyika kwa siku tatu ambapo Ofisi ya Mkemia Mkuu wa serikali imeandaa wataalamu ambao watawapitisha waganga wa tiba asili katika mada mbalimbali ambazo zinahusiana na kazi yao.


Naye Mganga wa Tiba asili kutoka wilaya ya Ukerewe Mkoani mwanza Dorkas Utepe ameipongeza serikali kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo itakuwa ni chachu ya mabadiliko Kwa waganga ambao walikuwa wakifanya kazi zao Kwa mazoea na kusababisha athali mbalimbali Kwa jamii.

No comments:

Post a Comment