TOENI TAARIFA PINDI MNAPOONA VIASHIRIA VYA UHALIFU-ACP MTALEMWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, January 10, 2023

TOENI TAARIFA PINDI MNAPOONA VIASHIRIA VYA UHALIFU-ACP MTALEMWA


Na Mwandishi wetu Dodoma 

Wafanyabiashara na wasafiri katika stendi kuu ya mabasi nanenane wamehimizwa kutoa taarifa juu ya uwepo wa wahalifu na uhalifu pindi wanapoona viashiria hivyo.

Akizungumza hii leo Januari 10,2023 katika kituo Cha mabasi Nane Nane kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Archelaus Mtalemwa, amesema ni wajibu wa kila mwananchi Katika kuhakikisha usalama unakuwepo kwa kutowaficha waharifu.


Amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma Katika kuhakikisha linakuwa karibu na wananchi, linaendelea kutoa Elimu, na kufanya wawe mstari wa mbele kuwatambua watu wanaofanya vitendo vya kiharifu ili kuendelea kuwa na jamii salama.

"Maeneo ya stendi Yana mkusanyiko wa watu wengi, watu wengine wanavuta bangi, wanauza madawa ya kulevya, wezi na mengineyo, tunachoomba wananchi mnaofanya shughuli hapa,muwe karibu na Jeshi la Polisi kuhakikisha mnatoa taarifa zitakazotuwezesha kuwapata hawarifu wanaowabughuzi na kuwatesa wananchi", amesema Mtalemwa.


Kwa upande wake Mabruk Seif, meneja wa Stendi Kuu ya Mkoa wa Dodoma, amelishukuru Jeshi la Polisi kwa kutoa Elimu ya uharifu na waharifu Katika eneo hilo.

Nao baadhi ya wafanyabiashara Katika stend hiyo wameomba zoezi la kutoa Elimu liwe endelevu ili kuhakikisha wananchi na Polisi wanashirikiana kwa pamoja Katika kuhakikisha ulinzi unaimarishwa na kutokomeza uhalifu.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma, limeshiriki Katika zoezi la kufanya usafi na kutoa Elimu juu ya uhalifu na wahalifu katika kituo Cha mabasi nanenane mkoani Dodoma.

No comments:

Post a Comment