Na Gideon Gregory-Dodoma
Ujumbe wa Tume hiyo ambao umezuru hapa nchini chini ya wenyeji wa tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora umewasilisha pongezi hizo na kusisitiza kuwa idhini ya Rais Dkt. Samia ya kufanyika kwa mikutano hiyo inatoa uhuru wa watu kujieleza na kutoa maoni yao.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji Mstaafu. Mathew Maimu amebainisha hayo jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kwa wanahabari juu ya ujumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Watu Afrika (ACHPR)
“Tumefikiria ni jambo jema kuwashirikisha nyinyi waandishi wa habari kwa maana nyie ni wadau wetu na tumekuwa tukishirikishana mambo mengi sasa leo tulivyopata huu ugeni tukaona ni vyema pia kushirikiana nanyi katika mambo machache ambayo wageni wetu haya wanataka kuyajua kutoka tume,”amesema Maimu.
Kuhusu Mpango wa Serikali wa kuwahamisha kwa hiari jamii ya watu waishio Loliondo ACHPR Imeshauri uwe mpango wa Kudumu ili kuendelea kulinda haki za binadamu nchini
Wajumbe hao wameambatana na watumishi wengine watatu wa tume huku dhumuni la ujio wao likiwa ni kukuza matumizi ya mkataba wa Afrika wa haki za Binadamu na Watu.
No comments:
Post a Comment