TUMIENI MIKOPO YA ASILIMIA 10 YA MAKUSANYO YA NDANI KUWAWEZESHA WAJASIRIAMALI -MAJALIWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, January 7, 2023

TUMIENI MIKOPO YA ASILIMIA 10 YA MAKUSANYO YA NDANI KUWAWEZESHA WAJASIRIAMALI -MAJALIWA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia makaa ya mawe, wakati alipotembelea Kampuni ya Jitegemee Holdings, Mdunduwalo, Luanda mkoani Ruvuma, Januari 07, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia bidhaa zinazozalishwa kutokana na makaa ya mawe na wanakikundi cha Mbalawala Women Organization, wakati alipotembelea kikundi hicho, Mdunduwalo, Luanda mkoani Ruvuma, Januari 07, 2023. Kutoka kulia ni Meneja wa Fedha Ester Mwamwezi na Meneja Uzalishaji wa Kikundi hicho, Rose Samweli. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia machine zinazotengeneza bidhaa za makaa ya mawe, kwenye Kikundi cha Mbalawala Women Organization, kilichopo Mdunduwalo, Luanda mkoani Ruvuma, Januari 07, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua shughuli za uchimbaji makaa ya mawe, katika Kampuni ya Jitegemee Holdings, Mdunduwalo, Luanda mkoani Ruvuma, Januari 07, 2023. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Emmanuela Kaganda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanakikundi cha Mbalawala Women Organization, wakati alipotembelea kikundi hicho, Mdunduwalo, Luanda mkoani Ruvuma, Januari 07, 2023. Kutoka kulia ni Meneja wa Fedha Ester Mwamwezi na Meneja Uzalishaji wa Kikundi hicho, Rose Samweli. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia moja ya bidhaa zinazozalishwa kutokana na makaa ya mawe, wakati alipotembelea Kikundi cha Mbalawala Women Organization, kilichopo Mdunduwalo, Luanda mkoani Ruvuma, Januari 07, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia machine zinazotengeneza bidhaa za makaa ya mawe, kwenye Kikundi cha Mbalawala Women Organization, kilichopo Mdunduwalo, Luanda mkoani Ruvuma, Januari 07, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Na Mwandishi wetu Ruvuma

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa Halmashauri zote nchini waweke mpango wa namna bora ya kuviwezesha vikundi vya wajasiriamali katika maeneo yao kupitia mikopo ya asilimia 10 ya makusanyo ya ndani ambayo itawawezesha kuendeleza miradi yao na kuleta tija.

“Badala ya kutoa mikopo ya fedha kidogo kidogo mnaweza kutoa fedha nyingi kwenye kikundi kimoja kimoja kama shilingi milioni 200 kukiwezesha kikundi husika kuanzisha mradi mkubwa ambao unaweza kuwaingizia fedha nyingi hivyo kuongeza tija”

Kadhalika Mheshimiwa Majaliwa amemtaka Meneja wa TARURA mkoa wa Ruvuma ashirikiane na Meneja wa TARURA wa wilaya ya Mbinga kufanya tathimini ya mahitaji ya matengenezo ya mtandao wa barabara katika maeneo ya uchimbaji wa makaa ya mawe na kuhakikisha zinapitika wakati wote ili kuwawezesha wawekezaji kufanya shughuli zao kwa ufanisi.

Ameyasema hayo leo (Jumamosi, Januari 7, 2023) baada ya kutembelea na kukagua shughuli za uchimbaji wa makaa ya mawe katika mgodi wa kampuni ya Jitegemee Holdings ulioko katika kijiji cha Mdunduwalo, Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma.

Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji hivyo ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) lihakikishe linafikisha umeme wa gridi ya Taifa katika migodi ya makaa ya mawe mkoani Ruvuma ili kuwapunguzia wawekezaji gharama za uendeshaji.

Akizungumza baada ya kutembelea kampuni ya makaa ya mawe ya Jitegemee holdings, Waziri Mkuu amezitaka Jumuiya za Chama cha Mapinduzi wilaya ya Mbinga kuwekeza katika utengenezaji wa nishati ya mkaa wa kupikia kwa kutumia makaa ya mawe ili kudhibiti ukataji wa misitu na kuhamasisha utunzaji wa mazingira.

Kampuni hiyo imefanikiwa kuchangia shilingi bilioni 7.01 katika pato la Taifa, kati yake shilingi milioni 81.73 zimelipwa kwa halmashauri kupitia tozo na ushuru mbalimbali na Shilingi Milioni 292 ni kodi nyingine za serikali ikiwemo PAYE, kodi ya zuio na SDL.
“Kampuni imeshalipa Mrabaha jumla ya kiasi cha Shilingi Bilioni 3.59 na shilingi milioni 488 kama ada ya vibali vya kusafirisha mkaa nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment