WATAALAM WA AFYA WATAKIWA KUWA NA MIKAKATI YA PAMOJA , KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA WATOTO. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, January 16, 2023

WATAALAM WA AFYA WATAKIWA KUWA NA MIKAKATI YA PAMOJA , KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NA WATOTO.


Na.Faustine Gimu,Elimu ya Afya Kwa Umma,Kilimanjaro.

Rai imetolewa kwa Wataalam wa Afya hapa nchini kuwa na mikakati ya pamoja itakayorahisisha kupunguza vifo vya mama na mtoto ,kwani katika takwimu za kitaifa zinaonesha kuwa kulikuwa na vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi kwa mwaka 2020 vilikuwa 1,640 na mwaka 2021 vilikuwa 1,588.

Rai hiyo imetolewa leo Januari 16,2023 mkoani Kilimanjaro na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu katika kikao cha wataalam wa Afya kanda ya Kaskazini kinacholenga kujadili namna ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga .

Mkuu huyo wa Mkoa ni muhimu wataalam wa Afya kujadili kwa kina kupunguza vifo vya akina mama na mtoto.

“Lengo la Serikali ya awamu ya sita ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kuhakikisha vifo vya mama na watoto havitokei hivyo ni muhimu ninyi kama madaktari na wataalam wa afya kuwa vifo vinapungua au kuisha kabisa”amesema .


Aidha,Mkuu huyo wa Mkoa wa Kilimanjaro amefafanua kuwa takwimu za watoto waliozaliwa wafu ni 17339 kwa mwaka 2019, huku kanda ya Kaskazini ilikuwa 150 mwaka 2020, vifo 175 mwaka 2019 na vifo 135 mwaka 2022.

Hali ya vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi kwa ngazi ya mikoa, vilikua mkuu huyo wa mkoa amesema ; mkoa wa Kilimanjaro; mwaka 2020 vifo 51, mwaka 2021 vifo 66 na mwaka 2022 vifo 39 huku Mkoa wa Arusha; mwaka 2020 vifo 46, mwaka 2021 vifo 55 na mwaka 2022 vifo 61 na mkoa wa Tanga; mwaka 2020 vifo 53, mwaka 2021 vifo 55 na mwaka 2022 vifo 35.

Takwimu za kitaifa zinaonyesha kuwa vifo vya watoto wachanga kwa mwaka 2021 vilikuwa 6,720. Idadi ya vifo vya watoto wachanga kwa kanda ya Kaskazini vilikuwa 1,229 mwaka 2019, vifo 1,015 mwaka 2020, mwaka 2021 vifo 1,189 na mwaka 2022 vifo 1,059.


Mkuu huyo wa mkoa ameainisha hali ya vifo vya watoto wachanga kwa ngazi ya mikoa ambapo ; mkoa wa Kilimanjaro; mwaka 2019 vifo 399, mwaka 2020 vifo 431, mwaka 2021 vifo 554 na mwaka 2022 vifo 430. Mkoa wa Arusha; mwaka 2019 vifo 459, mwaka 2020 vifo 386,
mwaka 2021 vifo 468 na mwaka 2022 vifo 420. Mkoa wa Tanga; mwaka 2019 vifo 209 mwaka 2020 vifo 189, mwaka 2021 vifo 204 na mwaka 2022 vifo 257.  

Pia,Mkuu huyo wa mkoa amehimiza kuwa na lugha staha kwa watumishi .

“Lugha yenye staha ni muhimu sana watumishi kuzingatia hali hii itasaidia kuendelea kuimarika kwa huduma za afya “amesema.

Afisa Programu Wizara ya Afya,Idara ya Afya ya Uzazi ,Mama na Mtoto Jackline Ndanshau amesema wao kama wataalam wa Afya wataendelea kuhakikisha wanatoa mafunzo kikanda huku mratibu wa Afya ya Uzazi,Mama na Mtoto Kanda ya Kaskazini Haikamesia Malisa akisema wataendelea kutoa huduma za afya kwa ueledi ili kupunguza vifo vya mama na mtoto.

Nao baadhi ya waratibu wa Afya ya Uzazi ,Mama na Mtoto akiwemo Fatina Rashid kutoka mkoani Kilimanjaro,Belinda Mumbuli kutoka mkoani Arusha pamoja na Peter Makichambo kutoka mkoani Tanga wamesema ni muhimu kukaa pamoja katika kuhakikisha vifo vya mama na mtoto havitokei.

 

Ikumbukwe kuwa sababu mbalimbali zinazochangia kuendelea kutokea kwa vifo vya akina mama vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga ni pamoja na kutokwa na damu nyingi kabla na baada ya kujifungua, kifafa cha mimba na madhara ya dawa za usingizi.

 Aidha, sababu zinazochangia vifo vya watoto wachanga ni pamoja na uambukizo mkali, kukosa hewa wakati wa kujifungua na madhara yatokanayo na kuzaliwa watoto njiti.

Sababu zote zilizoripotiwa na wataalam ambazo zilichangia vifo vya wajawazito na watoto wachanga zinahusiana na baadhi ya watoa huduma kutokuwa na ujuzi na uzoefu wa kutosha katika kukabiliana na dharura zinazojitokeza wakati wa uzazi hasa katika vituo vipya vilivyoanzishwa, ucheleweshwaji wa rufaa na ukosefu wa baadhi ya vifaa tiba vya dharura mfano machine za kutoa dawa za usingizi na ganzi. 

Kikao cha wataalam wa Afya kanda ya Kaskazini kinacholenga kujadili namna ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wachanga kimekutanisha katika mikoa ya Kilimanjaro,Arusha na Tanga huku kikienda sambamba na kaulimbiu isemayo.“uongozi na uwajibikaji ni chachu katika kupunguza vifo vitokananvyo na uzazi na watoto”

No comments:

Post a Comment