CHAGUZI ZA MAJUKWAA YA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI NGAZI ZA MIKOA UKOMO TAREHE 1, MACHI 2023 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, February 24, 2023

CHAGUZI ZA MAJUKWAA YA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI NGAZI ZA MIKOA UKOMO TAREHE 1, MACHI 2023


Na WMJJWM, Arusha

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju amemuagiza Mkurugenzi msaidizi Wa Maendeleo ya Jinsia Bi Rennie Gondwe kuhakikisha Mikoa yote ambayo haijafanya uchaguzi wa majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi ngazi ya mkoa kufanya hivyo kabla ya tarehe mosi mwezi Machi mwaka 2023

Wakili Mpanju ametoa agizo hilo wakati akifungua mkutano wa uchaguzi wa jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi Mkoani Arusha na kubainisha kuwa hadi sasa ni mikoa 16 kati ya 26 ndio imeshafanya chaguzi zake hali inayopelekea ucheleweshwaji wa uzinduzi wa Jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi la kitaifa 

Wakili Mpanju anasema katika kila mkoa ni lazima liwepo jukwaa ambalo wanawake watakutana kujadili ajenda zao na namna ya kuzifikia fursa mbalimbali za kiuchumi na kielimu ili kuweza kukua kiuchumi

  "Nikuagize Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya jinsia, hakikisheni mikoa yote ambayo haijafanya chaguzi za ngazi za mikoa, mikoa yote 26 ya Tanzania bara mpaka ifikapo mwisho wa mwezi wa pili hakikisheni wawe wameshafanya uchaguzi wa uwezeshaji wanawake kiuchumi ngazi ya Mikoa mabla ya mwezi Machi mwaka 2023" amesema Mpanju 


Wakili Mpanju akatumia fursa hiyo kuwasisitiza wale ambao watachaguliwa kuongoza majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi kwa ngazi za mikoa kuhakikisha wanakua mwangaza wa kuzivumbua fursa mbalimbali zitakazo wanufaisha wanawake kiuchumi 

"Nia ya smSerikali ni hayo majukwaa yatumike kuwakutanisha na watoa huduma mbalimbali wanaohitajika katika kuwawezesheni nyinyi kufanya shughuli zenu za kiuchumi, muweze kujua fursa gani za kiuchumi zipo ili muweze kuzifikia na kukuza kipato chenu na taifa kwa ujumla" amesema Mpanju

Aidha Wakili Mpanju anasema nia ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni kila mtu ashiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa taifa letu 

"Wakati anaanza kutuongoza Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu changamoto ilikua wanawake wengi walikuwa wameachwa nyuma kwenye nyanja zote ikiwemo eneo la kiuchumi na ndio maana mhe Rais akasema hapana pamoja na kwamba tuna miongozo Pamoja na kwamba tunazo sera akamalizia kwa kuunda Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum tusimamie eneo hili mahsusi na sisi hatukulaza damu na ndio maana mwaka jana tukazindua Mwongozo wa uwezeshaji wa wanawake kiuchumi " 
anasema Mpanju



Kwa Upande wake Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Sera, Mipango na uratibu wa Mkoa huo Deogratius Ruhamvya wakati kizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela, amesema kwa mujibu wa matokeo ya sensa ya mwaka 2022, wanawake wamechukua asilimia 61 ya wakazi wa mkoa huo, hivyo uwepo wa majukwaa hayo utasaidia kuwainua kiuchumi wanawake wengi wa mkoa huo

"Kwenye makundi yote haya upande wa marejesho kwa kweli tunakiri kundi kubwa la wanawake ndio linafanya vizuri kwa kurejesha kwa wakati na halisumbui, kwa hiyo tunatamani Majukwaa haya yaweze kukaa vizur na kufanya shughuli zake vizuri basi Serikali itaendelea kuweka fedha nyingi ambazo watarejesha na watainuka kiuchumi huku watu wengine wakiongezeka katika kunufaika na fedha hizi" amesema Ruhamvya


Nae Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa huo Bi Blandina Nkini katumia fusra hio kuwaasa wanawake na wapiga kura wa mkutano huo kuhakikisha wanachagua viongozi ambao watawasidia wanawake wa mkoa wa Arusha katika mlengo wa kuwainua kiuchumi.

No comments:

Post a Comment