Ambapo Mpaka dakika tisini zinakamilika Raja Casablanca imeizamisha simba kwa goli tatu kwa yai na inakuwa mchezo wa kwanza wa makundi ya klabu bingwa Afrika kwa simba kupoteza tangu ilivyoingia katika hatua ya makundi mwaka 2003.
Ikumbukwe kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan aliahidi zawadi ya Shilingi Milioni 5 kwa kila goli ambalo litafungwa na Timu ya Simba kwa maana hiyo simba wamepishana na mamilioni ya Dkt.Samia
Viongozi wengine walioshuhudia simba ikizamishwa kwa Mkapa ni Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mohamed Mchengerwa, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu na Katibu Mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi, Naibu Spika wa Bunge Mussa Hassan Zungu, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Ally Mayay na viongozi wengine.
No comments:
Post a Comment