TANZANIA YAPEWA TUZO YA UMOJA WA MARAIS WA AFRIKA WA KUPAMBANA NA MALARIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, February 18, 2023

TANZANIA YAPEWA TUZO YA UMOJA WA MARAIS WA AFRIKA WA KUPAMBANA NA MALARIA


Addis Ababa: Ethiopia

Serikali ya Tanzania imetunukiwa Tuzo ya Umoja wa Marais wa Afrika wa Kupambana na Malaria (African Leaders Malaria Alliance (ALMA) iliyopewa Jina la Joyce Kafanabo kuhusu Matumizi Mazuri ya Kadi Alama (ALMA Joyce Kafanabo Awards-Best Innovative Use of Scorecard Tools).

Tuzo hiyo imetolewa leo tarehe 18 Februari, 2023 katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika, Jijini Addis Ababa na Mhe. Generali Umaro Sissoco Embalo, Rais wa Guinea Bissau ambae pia ni Mwenyekiti wa ALMA na kupokelewa na Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Tanzania imetambuliwa kwa matumizi mazuri ya kadialama (Score Cards) kutokana na kufuatilia mwenendo wa ugonjwa wa malaria nchini katika ngazi zote za kutolea huduma za afya.

Bi. Joyce Kafanabo, ni Mtanzania na mmoja wa Wakurugenzi Waanzilishi ya Umoja wa Marais wa Afrika wa Kupambana na Malaria (ALMA) ulionzishwa chini ya Uenyekiti wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete mwaka mwaka 2009.


Tangu kuanzishwa kwake nchi nyingi za Afrika zimejifunza mengi kupitia Taasisi hii na kumekuwa na matumizi sahihi ya Kadialama katika kufuatilia utoaji wa huduma za ugonjwa wa malaria katika maeneo mbalimbali.


Sambamba na hilo, Tanzania imekuwa nchi ya mfano kwa kuwa na Chama cha Wabunge kinachosimamia ugonjwa wa malaria (TAPAMA) kupitia maeneo wanayotumikia wananchi.

No comments:

Post a Comment