MHE.GEKUL:VIPINDI VYA MICHEZO SHULENI VIZINGATIWE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, February 18, 2023

MHE.GEKUL:VIPINDI VYA MICHEZO SHULENI VIZINGATIWE


Na Shamimu Nyaki

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul amewaagiza Maafisa Utamaduni na Michezo kuhakikisha Vipindi vya michezo shuleni vinazingatiwa ili wanafunzi wapate nafasi ya kukuza vipaji walivyonavyo.

Mhe.Gekul ametoa agizo hilo Februari 18, 2023 mkoani Shinyanga wakati akifunga michezo iliyoandaliwa na Shule ya Sekondari Don Bosco Didia ambao ni wadau katika kukuza michezo kwa Wanafunzi.


Mhe. Gekul amesisitiza kuwa, Serikali chini ya Rais Dkt. Samia imerudisha michezo ya UMITASHUMTA na UMISSETA ili kuibua na kukuza vipaji vya watoto ambao ndio wanaotengeneza timu za Taifa, hivyo lazima wapate nafasi ya kucheza wanapokua shuleni.

" Kwenye Shule kuwe na maeneo ya michezo, na maeneo hayo yalindwe na yatunzwe ili watoto wapate sehemu ya kucheza, na sisi katika Serikali tumeshatenga Shule 56 ambapo hapa Shinyanga ni Shule ya Uhuru na Darajani" amesema Mhe. Gekul.


Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa huo Bibi. Daphrosa Ndalichako amesisitiza michezo yote ipewe nafasi ikiwemo fani za ndani zinazojumuisha ngoma, kwaya, maigizo na ngonjera.

Naye Mkuu wa shule hiyo Fr. Felix Francis Wagi ameishukuru Serikali kwa ushirikiano inayotoa kwa Shule hiyo katika mipango ya kuibua na kukuza vipaji

Michezo hiyo imeanza Februari 08 na imehusisha Riadha, mbio za baiskeli, netiboli, mpira wa miguu pamoja na maonesho ya Ubunifu.

No comments:

Post a Comment