Na Okuly Julius-Dodoma
Kutokana na ukuaji wa TEHAMA nchini,Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira Iringa (IRUWASA) imefanikiwa kuwafungia wateja 6,752 mita za maji za malipo kabla (prepaid Water Meters) na kuwa mamlaka inayoongoza kwa kufunga mita za maji za malipo kabla.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo Mhandisi David Pallangyo,wakati akielezea Utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Mamlaka hiyo leo Februari 27,2023,mbele ya waandishiwahabari,jijini Dodoma.
Mhandisi Pallangyo amesema kuwa kufungwa kwa mita hizo imesaidia kupunguza malalamiko kutoka kwa wanachi na imesaidia pia kuondoa ule urundikaji wa madeni ya maji.
"tunajivunia kuwa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira ya kwanza nchini kuwafungia wanachi wetu pamoja na taasisi mita za malipo kabla (prepaid Water Meters) na imetusaidia kuondoa malalamiko kutoka kwa wateja wetu pamoja na kupunguza ule mrundikano wa madeni sasa hivi hatuna tena migogoro na wateja wetu kwani unalipa unapata huduma,"amesema Mhandisi Pallangyo
Pallangyo amesema kuwa kupitia mfumo huo wa Malipo Kabla IRUWASA imefanikiwa kupunguza kiasi cha maji yasiyolipiwa kwa upande wa Iringa mjini kutoka wastani wa asilimia 24.6 mwaka 2020 hadi wastani wa asilimia 22.52 kwa mwezi Disemba 2022.
Pia Mhandisi Palangyo amesema kuwa idadi ya wateja waliounganishwa na majisafi imeongezeka kutoka 28,133 mwaka 2020 hadi 40,549 kwa mwezi Disemba 2022.
Pamoja na mafanikio hayo Mhandisi Pallangyo amezungumzia changamoto zinazoikabili mamlaka hiyo kuwa ni uchafuzi na uharibifu wa vyanzo vya maji ,kutokana na shughuli za kibinadamu zinazofanyika katika vyanzo hivyo kama vile kilimo,ufyatuaji wa matofali,ufugaji,uchimbaji wa michanga pamoja na ukataji wa miti,ambavyo vimekuwa vikipelekea kupungua kwa maji katika kina cha mto Ruaha mdogo hasa katika kipindi cha kiangazi.
"uchafunzi na uharibifu wa vyanzo vya maji imekuwa ni tatizo kubwa licha ya elimu inayoendelea kutolewa kwa jamii ila bado tatizo hili lipo ,niwaombe waandishi wa habari mtumie kalmu zenu vizuri kupanda na uharibifu huu wa vyanzo vya maji kwani tunatambua nyinyi mna uwezo huo na nguvu ya kuishawishi jamii kuachana na vitendo hivi,"amesisitiza Mhandisi Pallangyo
Changamoto nyingine ni uwepo wa mtandoa wa maji taka usiyokidhi mahitaji ambapo mfumo uliopo wa kukusanyia na kusafirishia majitaka umewafikia kwa asilimia 6.8 ya wakazi wa Iringa Mjini, wakati katika miji ya Kilolo na Ilula mfumo huo haupo kabisa.
Mamlaka ya Maji safi na usafi wa mazingira Iringa (IRUWASA),ilianzishwa mwaka 1998 ikiwa na jukumu la msingi la kutoa huduma endelevu za usambazaji majisafi na usafi wa mazingira kwa wakazi wa Manispaa ya Iringa ,ambapo mnamo mwaka 2020 IRUWASA iliongezewa maeneo ya kutoa huduma ya maji ya Ilula na Kilolo katika Wilaya ya Kilolo pamoja naeneo la pembezoni mwa Manispaa ya Iringa.
No comments:
Post a Comment