
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM),Dkt.Asha Rose Migiro,amezindua Shina la wakereketwa wa CCM Makunduchi lililopo Mtaa wa Uhuru Wilaya ya Dodoma Mjini,na kuwapongeza kwa kutumia shina hilo kama sehemu ya kujiongezea kipato bila ya kujali itikadi zao.
Akizungumza na wajumbe hao Januari 20,2026,kabla ya kuzungumza na Mabalozi wa Mashina wa Mkoa wa Dodoma,Dkt.Migiro,amesema hatua hiyo inaonyesha umoja na kudhihirisha kuwa kuna shughuli lazima ziwalete pamoja.
"Shina hili niwapongeze sana,mmetuthibitishia kuwa shughuli za kiuchumi hazina itikadi lakini katika kushirikiana hivi tunawavuta na kuwaleta pamoja watanzania,wanajamii wenzetu bila ya kujali itikadi kwa sababu maendeleo ya nchi hayana itikadi,umoja wa nchi hauna itikadi na umadhubuti wa Taifa pia hauna itikadi,"amesema.
"Ni jukumu letu kuhakikisha tushiriakana na jamii yote maana kura tulizopigiwa zimepigwa na wana CCM na wasio wana CCM.Na Rais wetu ambaye ni Mwenyekiti wa Chama chetu ni Rais wa wote hivyo na sisi lazima tuwe ni watumishi wa wote,"amesema.
Ametoa rai kwao kuwa mfano wa jamii kwa kupiga hatua mbele kimaendeleo.





No comments:
Post a Comment