Na Gideon Gregory, Dodoma.
Mratibu Makao Makuu kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Meshack Bandawe amesema kuwa serikali imetoa jumla ya viwanja 67 bure kwa balozi na mashirika mbalimbali ya umoja wa mataifa ili kuanza taratibu za kujenga ofisi zao makao makuu ya nchi jijini Dodoma.
Bandawe ameyasema hayo leo Februari 28, 2023 wakati akiwatembeza wageni kutoka ubalozi wa Norway nchini Tanzania walipofanya ziara yao ya kutembelea miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Tunafahamu ofisi za umoja wa mataifa, ubalozi wa Ujerumani, Ufaransa na China tayari umeanza kufungua ofisi zake Dodoma ili kurahisisha mawasiliano yake na serikali kwahiyo tumeamuwa kuwatembeza katika mji huu wa kiserikali ambao bado ujenzi unaendelea wa majengo 29 ambayo ujenzi wake umefikia 60%, tunatarajia kufikia mwezi Octoba ujenzi huu utakuwa umekamilika ambapo ghalama za mradi zitakuwa zaidi Bilioni 675, ”amesema Bandawe
Bandawe ameongeza kuwa ziara ya ubalozi huo kutembelea Dodoma ni sehemu ya mpango wa serikali kuhamia katika mji huo hususani ofisi za ubalozi na mashirika ya Umoja ya kimataifa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameukaribisha ubalozi huo kuhamia katika makao makuu ya nchi kwani zipo balozi nyingne zimeanza kuhamia.
“Balozi nyingine zimeshaanza kufungua ofisi zake na ubalozi wa mwisho kuhamia ulikuwa ubalozi wa Ujerumani,”amesema Senyamule.
No comments:
Post a Comment