OR TAMISEMI
Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo J. Dugange( Mb) hajaridhishwa na kasi ya ukusanyaji wa Mapato ya ndani katika halmashauri ya wilaya Longido ambapo kufikia tarehe 28 Machi 2023 wamekusanya bilioni 1.15 sawa na asilimia 41 ya lengo la makusanyo kwa mwaka.
Amebaini hayo leo tarehe 06 Machi 2023 wakati alipoanza ziara ya kikazi wilaya ya Longido mkoani Arusha na kupokea taarifa makusanyo ya mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2022/23.
Dkt. Dugange amesema katika mwaka wa fedha wa 2022/23 halmashauri ya wilaya Longido inatakiwa kukusanya bilioni 2.9 lakini hadi sasa wamekusanya asilimia 41 ya lengo la makusanyo.
Aidha, Dkt. Dugange amemtaka Mkurungenzi kuzingatia malekezo ya matumizi na mgawanyiko wa mapato ya ndani kulingana na mwongozo uliotolewa na Ofisi ya Rais TAMISEMI ikiwa ni pamoja na asilimia 40 ya miradi ya maendeleo na asilimia 10 ya Makundi maalum.
Amesema kati ya asilimia 40 ya mapato ya ndani iliyoelekezwa kupelekwa katika miradi hadi sasa wamepeleka asilimia 9 tu ya fedha iliyokusanywa jambo ambalo ni kinyumbe na Maelezo ya Serikali.
Vile vile, Amemtaka Mkurungenzi kuhakikisha anatenga na kupekeka asilimia 10 ya Mapato ya ndani katika vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu ambapo mpaka sasa halmashauri imepelekwa asilimia 6 kati ya 10 katika vikundi hivyo.
Ameagiza kufikia tarehe 30 Machi 2023 Halmashauri iwe imewasilsha Ofisi ya Rais TAMISEMI taarifa ya fedha ambazo zimepelekwa kukamilisha miradi ya maendeleo pamoja na vikundi maalum kulingana na Mwongozo ulivyoelekeza.
No comments:
Post a Comment