Na Mwandishi wetu Dodoma
Profesa. Mwamfupe aliyasema hayo jijini hapa wakati
akifungua mafunzo ya uboreshaji wa miliki wa adhi kwa
watendaji kata, madiwani, wenyeviti na wajumbe walioteuliwa na wananchi yaliyoandaliwa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Alisema lengo la serikali kutambulisha mradi huo ni kuondoa changamoto za migogoro ya ardhi inayowakabiri wananchi.
"Ninyi mliochanguliwa kuunda vikundi hivi kuanzia
madiwani,watendaji wa kata na mitaa pamoja na wajumbe
wamliopendekezwa hakikisheni mnawatenda haki kwa wananchi kwenye maeneo yao, msingeuke kuwa waporaji wa maeneo yao na mkifanya hivyo mtaondoa maana halisi la serikali kupitia wizara husika ambayo imetoa fedha nyingi kwa ajili ya mradi wa uboreshaji na upimaji"alisisitiza
Aidha aliwataka watumishi hao wakajikite pia kwenye kutoa elimu,itakayowafanya kushiriki kwenye mradi huo ambao utaleta matunda ya kiuchumi ukinzingatia kuwa wananchi wanaende kupimiwa maeneo yao na kupatiwa hati miliki itakayowasaidia kupata mikopo ya kifedha.
Katika hatua nyingine Profesa Mwamfupe alisema ili
kufanikisha mradu huo kunahitaji ushirikiano wa kutosha kati ya wizara na watendaji husika kwani baadhi ya wananchi wamekuwa na hofu ya kuporwa na maeneo yao yakiwemo viwanja,nyumba na mashamba.
Naye Meneja Mradi Urasimishaji Mjini, Leons
Mwenda alisema kuwa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi ni unaotekelezwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa muda wa miaka mitano ukiwa na dhumuni la kuongeza usalama wa milki kwa kutoa hati miliki 2,000,000 pamoja na hati miliki za kimila 500,000.
Alisema mradi huo utajenga ofisi za ardhi katika mikoa 25
ili kuendelea kusogeza huduma karibu na wananchi ikiwa ni
pamoja na kuboresha mifumo ya utunzaji taarifa za ardhi
pamoja na ukarabati wa ofisi za ardhi katika Halmashauri 41 nchini.
“Mradi huu ni jitihada za serikali ya Awamu ya sita katika
kuhakikisha usalama wa milki za ardhi unafikiwa na unalenga kuhakikisha migogoro ya ardhi inapungua na wananchi wanakuwa na uhakika wa kupata haki milki kwa maendeleo yao ambazo watazimia kwa kazi mbalimbali ikiwemo kuchukua mikopo kwa ajili ya kujiimarisha kiuchumi,”alisema
Aliongeza kuwa mradi huo utagharimu sh.bilioni 345 kwa nchi mzima na ukiwa na lengo la kuimarisha miundo mbinu ambayo itarahisisha huduma za ardhi ikiwemo ujenzi wa majengo katika mikoa 25 na kuboresha usalama wa milki za ardhi katika halmashauri saba , vijiji 250 na hati milki za kimila 500,000 .
Naye Diwani wa Kata ya Ng’ong’ona Loth Loth, alisema ardhi ndio uti wa mgongo wa wananchi hivyo mradi huo una manufaa kwa wananchi kwa kuwa ameufuatilia kwa karibu na kuona utekelezaji wake utakavyokuwa na kuwataka wananchi wa Mapinduzi B kuupokea namradi huo na kutoa ushirikiano.
MWISHO
No comments:
Post a Comment