SERIKALI YAZINDUA MRADI WA KUHAMASISHA ULAJI WA VYAKULA VILIVYOONGEZEWA VIRUTUBISHI SHULENI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, March 25, 2023

SERIKALI YAZINDUA MRADI WA KUHAMASISHA ULAJI WA VYAKULA VILIVYOONGEZEWA VIRUTUBISHI SHULENI


Na. Elimu ya Afya kwa Umma.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Bi. Mboni Mwita amezindua mradi wa kuhamasisha ulaji wa vyakula vilivyoongezewa virutubishi shuleni unaolenga kupunguza changamoto ya udumavu na upungufu wa madini na vitamini mwilini miongoni mwa wanafunzi na jamii kwa ujumla.

Uzinduzi huo umefanyika tarehe 23.03. 2023 Wilayani humo, ukishirikisha wadau mbalimbali ikiwemo Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na Wadau wa Maendeleo kutoka shirika la GAIN na SANKU.


Akizungumza katika uzinduzi huo, Mgeni rasmi Bi. Mboni alibainisha kuwa mradi huo utatekelezwa kwa miaka miwili kuanzia mwezi Februari 2023 hadi Machi, 2025 katika Mikoa ya kanda ya ziwa ambayo ni Kagera, Mwanza, Geita, Simiyu, Shinyanga na Mara.

Kwa upande wake: Msimamizi wa mradi huo kutoka shirika la SANKU, Bw. Gwao Omari, alisema "Takribani wanafunzi 120,000 kwenye shule 240, watanufaika na mradi huo kwa kuwawezesha kula chakula kilichoongezewa virutubishi pindi wakiwa shuleni ili kupunguza udumavu na upungufu wa vitamini na madini mwilini, ambapo kwa sasa changamoto hii ni kubwa kwenye Mikoa ya kanda ya ziwa"


Halikadhalika, Bw. Gwao alibainisha kuwa; wasagishaji wadogo 75 wa unga wa mahindi kutoka Mikoa hiyo watapatiwa mashine maalum za kuongeza virutubishi pamoja na kuwezesha wauzaji wa chakula shuleni walio chini ya utaratibu wa kawaida wa Serikali.

No comments:

Post a Comment