|
Mkurugenzi wa Kitengo ya Maadhimisho na Sherehe za Kitaifa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bw. Batholomeo Jungu (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika pita ya pamoja na kikosi kazi cha kitaifa cha kutembelea na kukagua ofisi za Serikali kuangalia utekelezaji wa maelekezo ya maadhimisho ya Sherehe za Miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na watendaji wa Benki Kuu Jijini Dodoma.Kauli mbiu ya maadhimisho mwaka huu ni “ Umoja wetu na Mshikamano ndiyo nguzo ya kukuza uchumi wetu.” |
|
Mkurugenzi wa Kitengo ya Maadhimisho na Sherehe za Kitaifa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bw. Batholomeo Jungu akitoa maelezo wakati wa ziara ya timu ya wataalam katika Jengo la Ofisi ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ikiwa ni ziara ya timu hiyo kukagua namna Ofisi za Serikali zilivyotekeleza maelekezo mahsusi ya namna ya kuadhimisha Miaka 59 ya Muungano Jijini Dodoma. |
|
Mkurugenzi wa Kitengo ya Maadhimisho na Sherehe za Kitaifa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bw. Batholomeo akizungumza na Timu ya watendaji wa PSSSF walipotembelea pamoja na timu ya wataalam kwa lengo la kukagua utekelezaji wa maelekezo ya kuadhimisha miaka 59 ya Muungango kwa ofisi za Serikali Dodoma. |
|
Timu ya wataalam ngazi ya Taifa yenye jukumu la kufuatilia maelekezo ya maadhimisho ya Sherehe za Miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Ofisi za Jeshi la Zimamoto mara baada ya ziara yao katika ofisi hizo.
|
|
Timu ya kikosi kazi Taifa cha kukagua utekelezaji wa maagizo mahsusi ya maadhimisho ya Sherehe ya miaka 59 ya Muungano ikiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukagua namna ofisi za Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi zilivyopamba jengo hilo Mtumba Dodoma. |
|
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Bi. Mary Maganga akimsikiliza Mkurugenzi wa Kitengo cha Maadhimisho na Sherehe za Kitaifa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Batholomeo Jungu wakati wa ziara ya kukagua namna Ofisi za Serikali zilivyoadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika ofisi zao zilizopo Mtumba Jijini Dodoma.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU) |
Na; Mwandishi Wetu – Dodoma
Kilele cha sherehe za Maadhisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Mwaka huu yamefanyika kiaina yake, ambapo kila mkoa unaadhimisha kwa kutelekeza maelekezo mahsusi ya Serikali.
Mkurugenzi wa Kitengo ya Maadhimisho na Sherehe za Kitaifa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Bw. Batholomeo Jungu ameyamesema hayo jana wakati ziara maalum ya Kamati ya Kitaifa ya maadhimisho hayo mwaka huu ilipotembelea na kukagua utekelezaji wa maelekezo mahsusi kwa Ofisi za Serikali Jijini Dodoma.
Bw. Jungu alisema kuwa kwenye mikoa ndipo kwenye wananchi hivyo shughuli hizi kufanyika katika mikoa zinaleta chachu ya uzalendo kwa wananchi sababu kila mtu anapata nafasi ya kushiriki kuanzia kwenye uzinduzi wa miradi, mashindano ya insha kwa wanafunzi, michezo mbalimbali, usafi wa mazingira na maswala mengine muhimu.
"Watu wapo katika kila mkoa, hivyo tukio hili la kushirikisha wananchi linaleta tija kwa jamii kwa kuona ni sehemu ya maadhimisho haya kwa vitendo,"alisisitiza Jungu.
Kwa Upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Bi. Mary Maganga aliseme
Kila mwaka tarehe 26 mwezi Aprili hututumika kama kumbukumbu ya sherehe za Muungano wa Iliyokuwa Tanganyika na Zanzibar, uliyofanya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, ambapo kaulimbiu ya Mwaka huu inasema “ Umoja wetu na Mshikamano ndiyo nguzo ya kukuza uchumi wetu.”
Katibu Mkuu Masanja alitumia fursa hiyo kueleza namna ofisi yake ilivyotekeleza maelekezo mahsusi ikiwemo kulipamba jengo la ofisi hiyo na kuweka picha za viongozi wakuu wa nchi pamoja na waasisi wa taifa leo.
No comments:
Post a Comment