Na Okuly Julius Dodoma
Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Kampuni ya Huawei International imesaini Mkataba wa Upanuzi wa mkongo wa Taifa wa Mawasiliano Katika Wilaya 23 nchini zenye jumla ya kilometa 1,520 wenye thamani zaidi ya bilioni 37 za kitanzania.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Waziri wa Habari, mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe.Nape Nnauye, amesema kukamilika kwa mradi huo kutafungua fursa kwa wananchi za kiuchumi, kwani Kasi ya upatikanaji wa mawasiliano yatachochea maendeleo Katika Wilaya hizo na Taifa kwa ujumla.
Waziri Nape amesema kutokana na uwepo wa changamoto ya ukosefu wa mawasiliano Katika baadhi ya maeneo, hali inayosababisha wananchi kukosa fursa mbalimbali za kijamii na kibiashara, serikali kupitia Shirika la mawasiliano Tanzania imeamua kuzitatua changamoto hizo kwa vitendo.
"Serikali Awamu ya sita inayoongozwa na Mhe Dkt Samia suluhu Hassan Rais Wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania imedhamiria kuhakikisha Tanzania inakuwa na miundombinu Bora ya mawasiliano yenye kutumia Teknolojia ya kisasa ambayo italeta tija na ufanisi katika kuongeza uzalishaji na ujenzi Wa uchumi pamoja na kuimarisha usalama na ulinzi Wa Taifa,"
Mhe.Nape amesema kuwa serikali imepanga kutekelwza Mradi Wa kuimarisha mawasiliano katika ngazi ya wilaya Kwa kuunganisha wilaya zote kwenye Mkongo Wa Taifa Wa amawailiano ili kuongeza Kasi ya upatikanaji Wa mawasiliano ambayo yatachochea Maendeleo katika wilaya na Taifa Kwa ujumla.
Na kuongeza kuwa "dhamira ya serikali ni kuhakikisha Mkongo wa taifa wa Mawasiliano unasambaa nchi nzima na nchi zote tunazopakana nazo ambapo kwa sasa tumebajisa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambayo mipango iliyopo ni kuifikia,"amesema Amesema Nnauye
Aidha,waziri Nape amesema kukamilika Kwa mradi huo Wa upanuzi Wa mkongo Wa Taifa Wa mawasiliano utasaidia kukuza matumizi ya TEHAMA na kuongeza Kasi ya upatikanaji Wa interneti yenye Kasi zaidi.
Waziri Nape pia ametoa rai katika maeneo yote yatakayopitiwa na mradi huo kuhakikisha wananchi wanapewa Elimu juu ya umuhimu wa miundombinu hiyo ili kila mmoja awe mlinzi wa mwenzake.
Awali akitoa Taarifa ya shirika la mawasiliano Tanzania (TTCL), Mkurugenzi mkuu Wa shirika hilo Mhandisi Peter Ulanga amesema kuwa upanuzi Wa mkongo huo Wa Taifa Wa mawasiliano kwa wilaya hizo 23 ,unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi sita na utasaidia katika kukuza shughuli za kiuchumi, kibiashara, kijamii sambamba na kuimarisha ulinzi na usalama ndani ya wilaya na mkoa.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Bi.Zuhura Muro amesema Serikali chini ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kuwezesha utekelezaji wa upanuzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwenda kwenye ngazi ya Wilaya inachochea maendeleo ya kiuchumi na kusaidia serikali kukusanya mapato kwa njia ya mtandao.
Mkataba huo ambao umesainiwa na TTCL na HUAWEI international unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi Cha miezi sita ambapo Wilaya 23 zitaungwa kwenye Mkongo huo ambazo ni Mkoa Wa shinyanga, halmashauri ya wilaya ya msalala,wilaya ya Mbogwe,wilaya ya Pangani,wilayaya Muheza,Kilindi,Mombo,Lushoto,halmashauri ya wilaya ya Ngara, Mwanga, Hai, Karatu, Longido, Mbulu,Kibiti,Mtama, Ruangwa, Nachingwea, Newala, Mbinga, Ludewa, Halmashauri ya Wilaya ya Vywawa na Wilaya ya ileje.
No comments:
Post a Comment