BUNGE LAIDHINISHA SHILINGI BILIONI 212.45 KUTUMIKA KATIKA BAJETI YA WIZARA YA HABARI KWA MWAKA 2023/24 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, May 19, 2023

BUNGE LAIDHINISHA SHILINGI BILIONI 212.45 KUTUMIKA KATIKA BAJETI YA WIZARA YA HABARI KWA MWAKA 2023/24


Na Okuly Julius-Dodoma

Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi Bilioni 212.457 Katika Mwaka wa Fedha 2023/24.


Ombi hilo limewasilishwa Bungeni na Waziri wa wizara hiyo Mhe.Nape Nnauye na kufafanua kuwa Kiasi cha zaidi Shilingi Bilioni  30.50ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ambapo zaidi ya Shilingi bilioni 18.52 ni za Mishahara na zaidi ya Shilingi  Bilioni 11.98 ni za Matumizi Mengineyo.



Huku zaidi ya Shilingi Bilioni 181.95 zinatumika  kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ambapo zaidi ya  Shilingi bilioni 146.777 ni Fedha za Ndani na zaidi ya  Shilingi bilioni 35.176 ni Fedha za Nje.


Akizungumza utekelezaji wa bajeti iliyopita Waziri Nape amesema Mwaka wa Fedha 2022/23 Wizara iliidhinishiwa kutumia kiasi cha Shilingi bilioni 282.06, Kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 26.3 ziliidhinishwa kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida na Shilingi bilioni 255.8 ziliidhinishwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.



Hata hivyo hadi kufikia mwezi Aprili, 2023 Wizara imepokea na kutumia jumla ya Shilingi bilioni 125.1. Kati ya fedha hizo Shilingi bilioni 12.8 sawa na asilimia 48.7 ya fedha za matumizi ya kawaida na Shilingi bilioni 112.3 sawa na asilimia 43.9 ya fedha za mendeleo.



No comments:

Post a Comment