Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma Octavian Bidyanguze,akizungumza wakati akifungua Jukwaa la Ushirika Mkoani Dodoma lililofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma Octavian Bidyanguze,akizungumza wakati akifungua Jukwaa la Ushirika Mkoani Dodoma lililofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square jijini Dodoma.
Na.Mwandishi Wetu-DODOMA
Wanaushirika mkoani Dodoma wametakiwa kutumia fursa za mafunzo yanayotolewa katika Jukwaa la Ushirika linalofanyika mkoani hapo ili kujiongezea maarifa na uwezo wa kuendesha na kusimamia kwa ufanisi shughuli za vyama vyao.
Akiongea katika ufunguzi wa Jukwaa la Ushirika Mkoani Dodoma katika Viwanja vya Nyerere Squire. Mrajis Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma Octavian Bidyanguze, amesema pamoja na mambo mengine Jukwaa hilo lina malengo ya kuwaongezea ujuzi kupitia mafunzo kutoka kwa wataalamu mbalimbali wanaoshiriki Jukwaa hilo.
Mrajis Msaidizi huyo amesema Jukwaa hilo linatekeleza kati ya Msingi wa Ushirika Kimataifa wa elimu, mafunzo na taarifa kwa kutoa Semina za mafunzo ya mada mbalimbali ikiwemo masuala ya Ushirika kwa Wanawake, Ushirika kwa vijana, Bima, kaguzi za Vyama pamoja na matumizi ya TEHAMA.
“Niwaombe wanaushirika mtumie fursa hii ya mafunzo kutoka kwa Wakufunzi na wataalamu wetu leo ili mpeleke ujuzi mtakaopata hapa kwa wanaushirika wengine katika vyama vyetu vya Ushirika,” alisisitiza
Aidha, katika mafunzo hayo Mratibu wa kanda ya kati wa Chuo cha Ushirika Moshi (MoCU) Bahati Rukiko amewakumbusha Wanaushirika kuwa na ushirikiano baina ya vyama ili kuendeleza na kuimarisha ushirika. Ameongeza kuwa Ushirikiano huo utasaidia kukuza masoko, kubadilishana uzoefu, kuongeza ubunifu na kujenga mahusiano baina ya vyama.
Mratibu amesema vyama vinapotekeleza dhana ya Ushirika kwa Ushirika vinapata fursa ya kutatua changamoto za wanaushirika ndani ya Ushirika akitoa mfano dhahiri wa Chama kimoja kuwa na uzalishaji mkubwa wa mazao bila masoko ya kutosha wakati chama kingine kikiwa na uwezo wa uchakataji wa mazao vishirikiane ili kuongeza thamani kuongeza wigo wa masoko.
Ameongeza kuwa ushirikiano baina ya vyama utasaidia vyama vya Ushirika vitasaidia kukuza vyama vidogo na vile vinavyoanza na kuvipa uwezo wa kukua na zaidi na hatimaye kuwa na vyama imara zaidi vyenye msaada kwa wanaushirika.
Maadhimisho hayo ya Jukwaa la Ushirika Mkoani Dodoma yanaadhimishwa kwa kauli mbiu isemayo “Ushirika kwa Maendeleo Endelevu” na yatahitimishwa Mei 19, 2023. Baadhi ya Vyama vya Ushirika vilivyoshiriki Jukwaa hilo ni pamoja na UDOM SACCOS, KKT Arusha Road SACCOS, MWASHITA SACCOS, Ushirika wa Wakulima wa Zabibu Mpunguzi (UWAZAMAM), MTAZAMO AMCOS (Bahi).
No comments:
Post a Comment