WAZIRI GWAJIMA :WAZAZI ACHENI KUTHAMINI MALI KULIKO WATOTO WENU. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, May 15, 2023

WAZIRI GWAJIMA :WAZAZI ACHENI KUTHAMINI MALI KULIKO WATOTO WENU.


Na Selemani Kodima-Dodoma

Ikiwa Leo Tanzania inaungana na Ulimwengu kuadhimisha Siku ya Familia,Wazazi wametakiwa kuacha kuthamini mali kuliko kuwajali watoto wao katika malezi .


Kauli hiyo Imetolewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,wanawake ,watoto na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima wakati akizungumza na Wakazi wa kata ya Chang'ombe kuhusu umuhimu wa siku ya familia na nafasi ya wazazi katika kulinda watoto na vitendo vya ukatili wa kijinsia.




Waziri Gwajima amesema kuwa ni muhimu wazazi na walezi kutambua familia inajengwa na kila mmoja hivyo ni muhimu kutenga muda wa kukaa chini na watoto wao na kuzungumza nao.


Aidha amesema kuwa wananchi wamekuwa wakipenda kulinda mali kuliko watoto wao hali ambayo ameitafsiri kuwa ni sawa na kupa nafasi shetani kumaliza familia.


Nae Mwenyekiti wa mtaa wa Chang'ombe Bw Abdalah Mtosa amewataka wazazi wahakikishie wanatafuta muda wa kukaa na watoto wao ili kufahamu madhila gani wanayapitia wakiwa majumbani na shuleni.


Wakati huo huo Waziri wa Maendeleo ya Jamii ,Jinsia ,wanawake ,watoto na Makundi Maalum Dkt Dorothy Gwajima alipata nafasi ya kutembelea baadhi ya familia katika mitaa ya Chang"ombe na kuzungumza na baadhi ya wanajamii kujua uelewa wao kuhusu siku ya familia na kutoa ufafanuzi kuhusu siku hii pamoja na masuala yanayofanywa na wizara hiyo kwa jamii.


Pamoja na dunia kuadhimisha siku ya familia leo Mei 15, Umoja wa Mataifa kwa upande wao unasema licha ya kwamba muundo wa familia unabadilika kote ulimwenguni kufuatia mienendo ya kimataifa na mabadiliko ya demografia lakini bado Umoja huo unatambua familia kama kundi msingi katika jamii.

No comments:

Post a Comment