NEEC NA ZEEA ZAINGIA MAKUBALIANO YA KUSHIRIKIANA KATIKA SHUGHULI MBALIMBALI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, May 11, 2023

NEEC NA ZEEA ZAINGIA MAKUBALIANO YA KUSHIRIKIANA KATIKA SHUGHULI MBALIMBALI

Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Tanzania (NEEC) Beng'i Issa (Kulia) na Mkurugenzi wa Wakala wa Baraza la Uwezeshaji Zanzibar(ZEEA), Juma Burhani Mohamed wakisaini makubaliano ya ushirikiano katika utekelezaji wa Shughuli mbalimbali.

Na Okuly Julius,Dodoma

Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Tanzania(NEEC) na Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar(ZEEA), zimetiliana saini makubaliano(MoU)
kwa lengo la kushirikiana katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali kwa kipindi cha miaka 3.


Akizungumza wakati wa kutiliana saini makubaliano hayo Leo Mie 11,2023,Jijini Dodoma, Katibu Mtendaji wa NEEC Beng'i Issa amesema wanaingia mashirikiano ili kuweza kufanya kazi kwa karibu, kwa pamoja na Zanzibar ili kuleta tija ya pande zote mbili.


Amesema Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji(ZEEF) inayosimamia Baraza hilo Zanzibar iliwasiliana na Baraza NEEC ili waweze kutoa maoni ya kuboresha, kushauri Wakala utakaoanzishwa Zanzibar watakaoanzisha uwe ya aina gani .


"Sisi ni Baraza wao ni wakala , hivyo tuko tofauti, Sheria zilizotuanzisha, hivyo tunaangalia mapungufu ambayo yalijitokeza kwetu ili kwao yasije yakajotokeza,"amesema Beng'i


Katibu huyo ametaja jambo lingine muhimu watakaloshirikiana kuwa ni suala la utafiti katika shughuli wanazofanya wanafanya tafiti, Sera za uwezeshaji na vile vile wanakuwa wanafanya tathmini, kwenye mambo kama hayo watashirikiana.


Pia amesema kuna miradi ya maendeleo ambayo mara nyingine inatoka nje, watu wa nje wanataka kufanya nao kazi hapa nchini, hivyo watakuwa wanashirikiana na taasisi hiyo ya Zanzibar, katika kutekeleza.



Amefafanua kuwa mashirikiano hayo kwa kuanzia yatakuwa ya miaka mitatu, hivyo wamesaini makubaliano Kwa ajili ya kushirikiana na baada ya miaka hiyo watajipima, wapi wamefanikiwa zaidi na wapi kuna changamoto ili waweze kuboresha zaidi.



Kwa upande wake Mkurugenzi wa Wakala wa Baraza la Uwezeshaji Zanzibar, Juma Burhani Mohamed amesema taasisi hiyo imewawezesha kiasi cha Sh. bilioni 17 kuwawezesha wananchi ili waweze kuniinua kichumi.


Buruhani amesema tayari wametengeneza ajira takribani 78000 Kwa wananchi wa Zanzibar yote hayo yamefanyika katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwa baraza hilo.



"Hivyo basi leo hii hapa kwa kusaini makubaliano (MoU) na Baraza la NEEC yanathibitisha muendelezo wa makubaliano tunayoingia na taasisi mbalimbali,"amesema.


Amesema katika kipindi kifupi chini ya usimamizi wa bodi ya wakurugenzi ya wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, taasisi imewwza kufanikiwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwa kutoa mafunzo, mikopo kwa wananchi zaidi ya 18493, kuendelea na shughuli za ulezi wa qajasiliamali kupitia kituo cha kulea wajasiamali Zanzibar.


No comments:

Post a Comment