Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Ahmed Abbas ,akizungumza wakati akifungua mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu marekebisho ya bei za maji za mamlaka ya maji Makonde, Wilayani Newala uliofanyika leo Mei 18,2023
Mkuu wa Wilaya Tandahimba Mhe. Kanali Patrick Sawala akisisitiza jambo wakati wa kufunga mkutano wa taftishi kuhusu maoni ya marekebisho ya bei za maji za mamlaka ya maji Makonde uliofanyika leo Mei 18,2023.
Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi EWURA . Bw. George Kabelwa akizungumza wakati wa taftishi ya maombi ya kurekebisha bei za maji za mamlaka ya maji Makonde, Wilayani Newala leo Mei 18, 2023.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Makonde, Mha. Francis Bwire akiwasilisha hoja ya maombi ya marekebisho ya bei za maji kwa wananchi na wadau , katika mkutano wa taftishi uliofanyika leo Mei 18,2023, Wilayani Newala.
Sehemu ya washiriki wakifatilia mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu marekebisho ya bei za maji za mamlaka ya maji Makonde, Wilayani Newala uliofanyika leo Mei 18,2023.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Ahmed Abbas ,akipokea mkoba wenye nembo ya EWURA kutoka kwa Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi EWURA . Bw. George Kabelwa mara baada ya kufungua mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu marekebisho ya bei za maji za mamlaka ya maji Makonde, Wilayani Newala uliofanyika leo Mei 18,2023.
Mkuu wa Wilaya Tandahimba Mhe. Kanali Patrick Sawala ,akipokea mkoba wenye nembo ya EWURA kutoka kwa Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi EWURA . Bw. George Kabelwa mara baada ya kufungua mkutano wa kukusanya maoni ya wananchi kuhusu marekebisho ya bei za maji za mamlaka ya maji Makonde, Wilayani Newala uliofanyika leo Mei 18,2023.
Na.Mwandishi Wetu-NEWALA
Wakazi wa Wilaya za Newala na Tandahimba mkoani Mtwara, leo 18 Mei 2023, wametoa maoni yao kuhusu mapendekezo ya bei mpya za maji za Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Makonde wakati wa mkutano wa taftishi uliofanyika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Newala.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali, Ahmed Abbas wakati akifungua mkutano huo, amewahimiza wananchi kutoa maoni kwa uhuru na umakini kwani uamuzi utakaotolewa na EWURA baada ya mchakato kukamilika utakua ni wa kila mmoja.
“ Kwanza niwapongeze EWURA kwa kuzingatia takwa la kisheria kutushirikisha kwenye suala hili muhimu,hivyo niwaombe kuwa huru kuchangia mjadala na kutoa maoni kwa ufasaha na maamuzi ya bei yatakapoletwa hapa yawe ni ya kwetu sote.”
Bw. George Kabelwa, aliyemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Dkt James Andilie katika mkutano huo, amesema kuwa,mantiki ya kuitisha mkutano huo ni kupokea maoni yatakayokuwa chachu ya EWURA kutoa uamuzi kwa kuzingatinga maslahi ya wananchi na watoa huduma.
“Ukusanyaji wa maoni ni njia ya kuwashirikisha kwenye masuala ya msingi yanayowahusu kama bei za maji.”
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Makonde, Mha. Francis Bwire, wakati akitoa hoja ya kuomba mabadiliko ya bei kwa wananchi, alisema kuwa, Mamlaka inakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa miundombinu na gharama kubwa za uendeshaji zinazofikia asilimia 90 ya mapato yake huku upotevu wa maji ukiwa zaidi ya asilimia 50; hivyo ongezeko la bei litasaidia kutatua changamoto hizo.
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba, Mhe. Kanali Patrick Sawala, ndiye aliyefunga mkutano huo na kuwasisitiza wananchi kuendelea kuwasilisha maoni kwa njia ya maandishi kwa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, S LP 2857, Dodoma au katika ofisi ya EWURA Kanda ya Mashariki, Dar es Salaam kabla ya tarehe 22 Mei 2023.
Mamlaka ya Maji Makonde inahudumia Wilaya mbili za Newala na Tandahimba, na wananchi zaidi ya 80 walihudhuria mkutano na kutoa maoni yao.
No comments:
Post a Comment