TAEC YABORESHA HUDUMA ZAKE JIJINI MWANZA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, May 22, 2023

TAEC YABORESHA HUDUMA ZAKE JIJINI MWANZA.


Serikali kupitia Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) inaendelea na ujenzi wa ofisi mpya pamoja na maabara katika Kata ya Mkolani Wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza.


Mkuu wa Ofisi ya Kanda ya Ziwa, Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania Bwn. MIGUTA NGULIMI amesema dhamira ya serikali ni kusogeza huduma karibu na wananchi na kukamilika kwa ujenzi huo kutasaidia huduma za vibali vya mionzi pamoja na ukaguzi wa watumiaji wa vyanzo vya mionzi.


Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania Bwn. PETER NGAMILO amesema uboreshaji wa ofisi unaendelea maeneo mbalimbali nchini ili kusogeza huduma karibu na wananchi.

No comments:

Post a Comment