TTCL KUONGEZA MAENEO ZAIDI YA KUTOA HUDUMA NCHINI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, May 13, 2023

TTCL KUONGEZA MAENEO ZAIDI YA KUTOA HUDUMA NCHINI

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL),Mhandisi Peter Ulanga (Kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano Kwa Wote (UCSAF ) (kulia),Justina Mashiba wakitia Saini mikataba ya kupeleka huduma ya mawasiliano vijijini baina ya UCSAF na watoa huduma za mawasiliano iliyofanyika Leo Mei 13,2023, Jijini Dodoma.


Na Okuly Julius- Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL),Mhandisi Peter Ulanga amesema Serikali kupitia Shirika hilo inatarajia kujenga minara 104 kwenye Kata 104 maeneo ya vijijini na kueleza kuwa huduma hiyo itaboresha mawasiliano na kuwa kichocheo Kwa kiuchumi.




Amesema kwenye zabuni hizi za Leo ambazo Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) imesaini na Mfuko wa Mawasiliano Kwa Wote (UCSAF) imewaongezea maeneo mengine 104 mbali ya yale maeneo 130 ambayo Shirika hilo ni mtoa huduma pekee Kwa sasa.



Mkurugenzi huyo ameeleza hayo leo Mei 13,2023 mara baada ya Hafla ya Kutia Saini mikataba ya kupeleka huduma ya mawasiliano vijijini baina ya UCSAF na watoa huduma za mawasiliano iliyofanyika Jijini Dodoma.


Mhandisi Ulanga amesema kuwa Shirika hilo litaendelea kushurikiana na watoa huduma wengine wa mawasiliano ili kuhakikisha mawasiliano yanakuwa Bora Huku akibainisha kuwa hata kule ambako hawajashinda zabuni watashiriki kuboresha huduma zao.


"Najua Kuna maeneo hatujashinda zabuni ila hata kama hatujashinda sisi ni watoa huduma Kwa wananchi hivyo tutashirikiana kuweka mitambo yetu na sisi ili kuboresha huduma zetu kwani tunapaswa kuchochea maendeleo katika uchumi wa kidijitali"amesema Mhandisi Ulanga


Aida, Mhandisi Ulanga ameongeza kuwa katika zabuni hiyo Serikali imewapatia ruzuku ya Bilioni 5 ambapo nao kama Shirika wataongeza kuhakikisha Ujenzi wa monara hiyo inakamilika ili wananchi waishio maeneo ya vijijini waanze kupata huduma.




Amesema huduma za TTCL zinapatikana kila palipo na ofisi za Shirika
la Posta na kuendelea kufanya maboresho ili
kuhakikisha huduma linazotoa zinakidhi viwango kwa kuboresha
mitambo na kuongeza vituo vya huduma kwa wateja.


Kwa upande wa huduma kwa wateja amesema maboresho yaliyofanyika ni pamoja na
kuhakikisha kituo cha huduma kwa wateja (call center) kinakuwa
thabiti na kupatikana ndani ya muda stahiki;



Sambamba na hayo amesema shirika
linaendelea kutoa elimu kwa wananchi kutumia huduma ya mawasiliano na kutoa
huduma ya njia ya mawasiliano (capacity service) na huduma ya
maunganisho (interconnect) nje ya nchi na kufanikiwa kutanua wigo wa huduma kwa wateja.



Naye Mtendaji Mkuu wa UCSAF Justina Mashiba amesema katika kuhakikisha wanafikisha huduma ya mawasiliano vijijini wanaenda kujenga minara 758 katika kata 713.


Amesema katika mkataba huo wanaenda kuongea nguvu minara 304 ambayo ilikuwa inatoa huduma ya 2G sasa itaanza kutoa huduma kwa 3G na maeneo mengine 4G.



“Lengo kubwa la kuanzisha UCSAF ni kupeleka mawasiliano maeneo ya vijijini na kuhakikisha watanzania wanapata huduma ya mawasiliano bila vikwazo ambapo katika kuhakikisha hilo hadi sasa tumeshajenga minara nchi nzima .


Ameongeza kuwa :”USCAF Imepeleka vifaa vya TEHAMA katika shule za umma ambapo hadi sasa tumepeleka katika shule 4750.pia tunaendelea na mradi wa tiba mtandao lengo ni kuhakikisha watanzania wanapata huduma bila kwenda Hospitali.


No comments:

Post a Comment