TUME YA HAKI ZA BINADAMU (THBUB) KUANZA UCHUNGUZI WA KIFO CHA MWANAFUNZI WA UDOM BI.NUSURA ABDALLAH - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, May 10, 2023

TUME YA HAKI ZA BINADAMU (THBUB) KUANZA UCHUNGUZI WA KIFO CHA MWANAFUNZI WA UDOM BI.NUSURA ABDALLAH


Na Okuly Julius-Dodoma

Tume ya haki za Binadamu na utawala Bora imetangaza kuanza Uchuguzi wa kifo cha mwanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Bi Nusura Hassan Abdallah ambaye alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya faraja mkoani Kilimanjaro.


Taarifa ya Tume ya haki za Binadamu na Utawala Bora iliyotolewa leo Mei 10,2023 na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu Mathew Mwaimu amesema kwa kipindi cha hivi karibuni tume ya haki za Binadamu na utawala bora imeona katika vyombo vya habari zikihuisha ajali ya Naibu Waziri wa OR-TAMISEMI, Dkt Festo Ndugange na kifo cha Nusura Abdallah .



Jaji Mstaafu Mwaimu amesema taarifa hizo za vyombo vya habari zimeoneakana kukinzana kutokana na taarifa zilizotolewa na jeshi la Polisi,Chuo kikuu cha Dodoma , Hospitali ya Faraja iliyopo Himo Mkoani Kilimanjaro na taarifa za wananchi kupitia mitandao ya kijamii.


Aidha Jaji Mstaafu Mwaimu amesema Tume inapoona kumetokea mashaka kutoka kwa wananchi kuhusu jambo lolote linaloashiria uvunjwaji wa haki za binadamu au mashaka ya haki kutokutendeka ina mamlaka ya kufanya uchuguzi juu ya jambo hilo.


Hivyo amesema kwa mujibu wa katiba na sheria za Tume wana jukumu la kutetea na kulinda haki za binadamu nchini.



"Kwa Mujibu wa kifungu cha 15 (1) cha sheria ya tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora sura ya 391 tume inayo mamlaka ya kuanzisha uchunguzi wake wenyewe juu ya malalamiko yanyoashiria uvunjifu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora pasipo kusubiri kuletewa malalamiko"


Pamoja na hayo amesema Tume imeazimia kufanya uchuguzi wake huru kwa madhumuni ya kubaini ukweli kuhusu matukio hayo.

No comments:

Post a Comment