Dkt. Yonazi aongoza Kikao cha Makatibu Wakuu cha Nishati Safi ya Kupikia - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, May 10, 2023

Dkt. Yonazi aongoza Kikao cha Makatibu Wakuu cha Nishati Safi ya Kupikia

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akiongoza kikao cha Kamati ya Uongozi kuhusu nishati safi ya kupikia kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma.
Wajumbe wa kikao cha Kamati ya Uongozi kuhusu nishati safi ya kupikia wakifuatilia mawasilisho wakati wa kikao hicho.
Naibu Katibu Mkuu Nishati Bw. Athuman Mbuttaka akizungumza jambo wakati wa kikao cha Kamati ya Uongozi kuhusu nishati safi ya kupikia kilichofanyika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma.
Wajumbe wa kikao cha Kamati ya Uongozi kuhusu nishati safi ya kupikia wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguzi wa kikao hicho Jijini Dodoma.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

NA.MWANDISHI WETU - DODOMA

KATIBU Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Dkt. Jim Yonazi ameongoza Kikao cha Kamati ya Uongozi ngazi ya Makatibu Wakuu kilicholenga kupitia utekelezaji wa maboresho ya rasimu ya Dira ya Taifa ya kuhamia katika matumizi ya Nishati safi ya kupikia 2033 na rasimu ya Mpango Mkakati wa Utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Nishati Safi ya Kupikia 2033 yaliyotolewa na Waziri Mkuu wiki moja iliyopita Machi 23, 2023 Mkoani Dodoma.


Dkt.Yonazi ameongoza Kikao hicho kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ngazi ya Makatibu Wakuu ambaye ni Katibu Mkuu Kiongozi.


Kikao hicho kimehusisha Makatibu Wakuu kutoka Wizara mbalimbali akiwemo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Athumani Mbuttuka na Wajumbe wa Kikundi Kazi cha Taifa cha Nishati Safi ya Kupikia kilichofanyika Machi 30, 2023 Jijini Dodoma.


Dkt. Yonaz amesema kuwa kikao hicho ni mahsusi kwa ajili ya kupitia utekelezaji wa maboresho na maelekezo yaliotolewa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, alipokutana na Mawaziri na Naibu Mawaziri Machi 23, 2023 Mkoani Dodoma.


Mara baada ya Makatibu Wakuu hao kupitia Rasimu ya Dira ya Taifa ya kuhamia katika matumizi safi ya Nishati Safi ya Kupikia 2033 na Rasimu ya Mpango Mkakati wa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Nishati Safi ya Kupikia, itawasilisha kwa Waziri Mkuu tarehe 31 Machi 2023.

No comments:

Post a Comment