WAZIRI AWESO:HAKUNA KISINGIZIO MRADI UKAMILIKE KWA WAKATI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, May 5, 2023

WAZIRI AWESO:HAKUNA KISINGIZIO MRADI UKAMILIKE KWA WAKATI.


Na Okuly Julius-Dodoma

Waziri wa Maji Mhe.Juma Aweso amemuagiza Mkandarasi wa Mradi wa Visima vya Maji Nzuguni kuhakikisha wanatekeleza mradi huo bila kuleta visingizio baada ya Malipo ya awali kufanyika .


Pia amesema mradi huo unatakiwa kukamilika ifikapo mwezi wa nane mwaka huu.



Maagizo hayo ameyatoa leo wakati wakipokea mabomba ya maji katika eneo la mradi Nzuguni Jijini Dodoma ambapo amemuagiza Mkurugenzi wa Mtendaji wa Duwasa kuhakikisha mradi huo hauna Visingizo vyovyote na kuhakikkisha vifaa vinavyotakiwa kwenye mradi huo vinaagizwa mapema.


Aidha ameagiza utafiti uendele kufanyika ili kugundua na kuongeza visima Vingi vya maji.



Kwa upande wake katibu mkuu wizara ya maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba amesema watahakikisha wanafanya malipo kwa wakandarasi ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati.


Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Duwasa Mhandisi Aron Joseph akitoa taarifa juu  ya mradi huo amesema mradi umefikia asilimia 37.5 ambapo ni hatua ya ujenzi wa vibanda,mitaro ya kusimika mabomba ya maji .


Mhandisi Aron amesema tayari wamefanya malipo ya awali kwa wakanadarasi wa mradi huo hivyo wanategemea ndani ya miezi sita hadi nane kukamilika kwa mradi huo wa maji.



Kwa upande wake Mstahiki Meya wa jiji la Dodoma na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Maji DUWASA Prof Davis Mwamfupe amesema kupitia mradi huo wa maji wananchi wa Nzuguni wamekuwa na Mwamko mkubwa na kuahidi kuwa wataendelea kuwa Bega kwa Bega na DUWASA katika kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.


Diwani wa kata ya Nzuguni Aloyce Luhega amesema kupitia mradi huo ni historia ya wananchi wa Nzuguni kutokana na eneo hilo tangu uhuru halijawahi kuwa na chanzo cha maji safi na salama .


Nao baadhi ya wananchi wa kata ya Nzuguni wamesema uwepo wa mradi huo ni hatua kubwa ya kuwapunguzia adha ya maji ambapo walikuwa wakitumia maji ya visima yasio safi na salama na itawapunguzia umbali wa kufuata huduma ya maji .


Itakumbukuwa kuwa Mradi wa visima vya maji Nzuguni unatarajia kukamilika mwezi wa nane mwaka huu na unatarajiwa kuhudumia wakazi wa nzuguni,Ilazo na maeneo ya jirani ya kisasa na kupunguza adha ya maji katika maeneo hayo.

No comments:

Post a Comment