WIZARA YA KILIMO KUIMARISHA SEKTA YA KILIMO ILI KUENDELEA KUWAVUTIA VIJANA NCHINI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, May 11, 2023

WIZARA YA KILIMO KUIMARISHA SEKTA YA KILIMO ILI KUENDELEA KUWAVUTIA VIJANA NCHINI.


Na Gideon Gregory, Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Dkt. Hussein Mohamed amesema kuwa serikali kupitia wizara hiyo imelenga kuimarisha sekta ya kilimo ili kuendelea kuwavutia vijana nchini kujikita katika kilimo biashara ili kuondokana na dhana ya kusubilia kuajiriwa serikalini.


Dkt. Mohamed ameyabainisha hayo leo Mei 11,2023 katika hafla ya uzinduzi wa
mradi wa kuimarisha Sekta binafsi (Feed the Future Tanzania uliopo chini ya shirika la maendeleo la kimataifa la Marekani (USAID).


Amesema kuwa ushiriki wa sekta binafsi unahitajika kutokana na ukubwa wa nchi na wahitaji kuongezeka licha serikali kuwa kubwa lakini haiwezi kufika kila maeneo hapa nchini.


“Tunaamini kupitia sekta binafsi tutapata ugunduzi mkubwa kwa kushirikiana na sekta mbalimbali nchini katika kuiletea maendeleo nchi yetu pia katika kueneza matumizi ya sayansi na teknolojia itakuwa rahisi na hili litachangia kukua haraka kwa nchi kwa maana kuzingatia ajenda yetu ya 20/30 kuhakikisha kilimo kinakuwa kwa 10%,”amesema.


Amesema mradi huo utachangia katika kutekeleza dira ya maendeleo ya 2030, na kuongeza kuwa Tanzania kwasasa ina takribani vijana milioni 16 na muongo mmoja uliopita vijana wengi walikuwa wanategemea ajira kutoka serikalini na Wizara imeamua kutengenezea mazingira ya kujiajiri kupitia sekta ya kilimo.


“Tumekuwa na programu nyingi za kuhakikisha ili linafanikiwa kwa kufanya vijana wengi kuacha kutegemea ajira za serikali na lengo la wizara ni kuhakikisha kilimo kinawavutia vijana wengi na wao wanaingia kwenye kilimo,”amesema.


Dkt. Mohamed ameongeza kuwa wakifanikiwa kuboresha kilimo na kuwavutia vijana wataweza kuisaidia serikali kwenye utegemezi wa ajira wanapotoka vyuoni.



Kwa upande wake Meneja wa Justin Natural Honey Bw. Justin Mgeni mfugaji wa nyuki, amesema kuwa baada ya kuhitimu elimu ya chuo akuhitaji kusubiria suala la ajira aliamuwa kujikita katika ufugaji wa Nyuki.


Amesema lengo kuu lililo msukuma kufanya hivyo ni baada ya kuona kuna changamoto ya ufungashaji, ukosefu wa kupata bidhaa bora za mazao ya Nyuki na kuamaua kuleta vifaa mbalimbali ili kukabiliana na suala hilo.


“Pia niliona kuna changamoto ya kupata ajira lakini vijana wengi wanaweza kujikita huko, kwa hiyo ilikuwa ni njia pekee ya mimi kukabiliana na changamoto ya ajira baada ya kuhitimu chuo,”amesema.


Ameongeza kuwa kupitia Mradi wa Feed the Future utawasaidia kujulikana zaidi na kuifanya shughuli yake kuwa rasmi kutokana na kukosa baadhi ya vitu kutokana na suala la mtaji.



Naye Mkurugenzi wa SANAVITA. CO. LTD Jolenta Joseph, Kampuni inayohusika na kukabiliana na Utapiamlo, ameiomba serikali kuhakikisha inaweka wazi kila kitu pale wanapokuwa wanasajili kampuni ikiwemo suala la kulipia kodi ili kuepusha migongano inayoweza kujitokeza wakati shughuli zikiwa zinaendelea.


“Tunaishukuru serikali kwa kutuletea mradi wa BBT, kwani umeweza kuwainua vijana wengi kukabiliana na changamoto ya ajira, pia na huu mradi wa Feed the Future utaweza kutufungulia njia ya kujitangaza zaidi ndani na nje ya nchi, na endapo serikali itaendela kuwekeza nguvu kwa vijana naamini malengo ya Ajenda 20/30 tutayafikia,”amesema.


No comments:

Post a Comment