DKT.KIKWETE AMPONGEZA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, June 27, 2023

DKT.KIKWETE AMPONGEZA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya Nne Dkt.Jakaya Kikwete ,ambaye pia ni Mwenyekiti wa taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na Masuala ya Maji Barani Afrika (Global water Partnership-Southern Africa and Africa Coordination Unit na Mwenyekiti mwenza Mbadala alternat Co-chair wa AIP High level panel, akizungumza na watumishi wa Wizara ya Maji Juni 26,2023, Jijini Dodoma.


Na Okuly Julius-Dodoma

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya Nne Dkt.Jakaya Kikwete ameipongeza Serikali ya awamu ya Sita Inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan Kwa kuendelea kukamilisha Miradi ya Maji ikiwemo Program ya uwekezeji wa Maji (TanWIP).


Pia ameitaka Wizara ya Maji kuhakikisha wanakamilisha miradi ya maji ambayo haikukamilika katika awamu zilizopita ili kukamilisha azma ya Serikali ya kuhakikisha Kila mwananchi anapata maji Kwa umbali usiozidi mita 400.


Dkt.Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa taasisi ya kimataifa inayojishughulisha na Masuala ya Maji Barani Afrika (Global water Partnership-Southern Africa and Africa Coordination Unit na Mwenyekiti mwenza Mbadala  alternat Co-chair wa AIP  High level panel, ametoa kauli hiyo Leo Juni 26,2023 wakati akizungumza na watumishi kutoka Idara mbalimbali ya sekta ya maji kuhusu Mradi wa uwekezaji wa Maji (TanWIP).

Ambapo ameitaka Wizara ya Maji kuhakikisha wanakamilisha miradi ya maji ambayo haikukamilika katika awamu zilizopita ili kukamilisha adhma ya Serikali ya kuhakikisha Kila mwananchi anapata maji Kwa umbali usiozidi mita 400.


Ambapo amewataka kuendelea kuendelea kuchapa kazi ili kuhakikisha watanzania wanapata huduma ya maji.


Pia ametoa wito Kwa Waziri wa Maji na watumishi wote wa Wizara hiyo kuhakikisha wanakamilisha kile ambacho yeye kipindi akiwa Waziri wa Maji na Mpaka anakuwa Rais alishindwa kukikamilisha.


"Niwaombe sana Kuna kile ambacho sisi tulishindwa kukikamilisha kipindi tukiwa madarakani hivyo naamini Chini yako Waziri Jumw Aweso Kwa kushirikiana na Hawa watumishi wenzako mtakamilishi,"amesema Dkt.Kikwete


Kwa upande wake Waziri wa Maji Jumaa Aweso amewataka watumishi wa Sekta ya Maji kutumia vyema nafasi wanazopata kwa kutenda wema Kwa Wananchi isiwe ni sehemu ya kujitutumua na kuwaumiza wengine.


Pia amewataka kuhakikisha wanatumia nafasi zao Kwa weledi Mkubwa kuhakisha lile Jukumu walilopewa la kumshusha mama ndoo Kichwani linakamilika kisawasawa.



Pia amesema Wizara ya Maji itaendelea kuwatumia Viongozi Wastaafu Kwa sababu tayari wanaijua tulipotoka ,tulipotoka na wana ndoto hivyo ni vyema kuhakikisha tunawatumia vyema ili kufikia malengo kama taifa.


Amesema Programu ya uwekezaji katika sekta ya maji ni kubwa hivyo itatumia mito mikubwa ,Maziwa na kuhakikisha maji yanapatikana Kwa watanzania na unatarajiwa kukamilika ifikapo 2030.

No comments:

Post a Comment