Angela Msimbira Tabora
Mikoa ya Manyara na Katavi imeanza vema Michezo ya Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) inayoendelea mkoani Tabora.
Katika michezo iliyochezwa mapema leo 04 Juni 2023, Timu za wavu ya wasichana kutoka Mikoa ya Katavi na Mwanza zilikutana katika viwanja A katika shule ya Sekondari Tabora wavulana.
Mchezo huo wa kuvutia uliisha kwa Mkoa wa Katavi kuibuka na ushindi wa seti 3 kwa 0, hivyo kuashiria dalili njema katika mashindano hayo ambayo yameingia siku ya pili.
Katika mchezo mwingine timu ya Mkoa wa Manyara imeibuka na ushdi dhidi ya Dar-es-Salaam, kufuatia ushindi wa Seti 3-0 na hivyo kuifanya Mkoa wa Manyara kuanza vema mashindano kwa upande wa mpira wavu wasichana.
Kwa upande wa wavulana, mchezo wa awali ulizikutanisha timu kutoka Mikoa ya Pwani na Katavi, na kushuhudiwa Pwani ikishinda seti 3 kwa 1, huku Lindi ikishinda 3-1 dhidi ya Shinyanga.
No comments:
Post a Comment