MHE.SIMBACHAWENE AITAKA TAKUKURU ISIJIFUNGIE OFISINI, IENDE KWA JAMII - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, June 15, 2023

MHE.SIMBACHAWENE AITAKA TAKUKURU ISIJIFUNGIE OFISINI, IENDE KWA JAMII

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akizungumza na Maafisa wa TAKUKURU wakati alipowatembelea katika ofisi zao zilizopo jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Sehemu ya Maafisa wa TAKUKURU wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene wakati alipowatembea katika ofisi zao zilizopo jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Kamishna wa Polisi, Salum Hamduni akielezea utekelezaji wa majukumu ya ofisi yake kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene wakati alipowatembelea katika ofisi za TAKUKURU zilizopo jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene kuzungumza na Maafisa wa TAKUKURU Katika ofisi zao zilizopo jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akipokea nakala ya Mwongozo wa TAKUKURU Rafiki kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Hamduni wakati wa ziara ya kikazi kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji. Kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete wakiwa wamekabidiwa maua ikiwa ni ishara ya ukaribisho wao katika ofisi za Dodoma za TAKUKURU
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja baada ya kuhitimisha kikao kazi chake na maafisa wa TAKUKURU alipowatembelea katika ofisi za Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete moja ya vitendea kazi vya TAKUKURU kutoka Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU CP. Salum Hamduni wakati wa ziara ya kikazi kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha ya pamoja baada ya kuhitimisha kikao kazi chake na maafisa wa TAKUKURU alipowatembelea katika ofisi za Dodoma kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji.


Na. Veronica Mwafisi-Dodoma
Tarehe 15 Juni, 2023


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. George Simbachawene amewataka Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kutoka ofisini na kwenda sehemu ambako huduma za kijamii zinatolewa kwa kuwa huko kuna malalamiko mengi ya wananchi kuhusu kutondewa haki katika kupata huduma.


Mhe. Simbachawene ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati wa kikao kazi chake na Watumishi wa Taasisi hiyo kilicholenga kuhimiza uwajibikaji katika kutekeleza majukumu yao kwa maslahi mapana ya Taifa.


Amesema ni wakati sasa wa TAKUKURU kwenda kupambana na rushwa katika maeneo hayo badala ya kukaa ofisini huku wakisubiri kupewa taarifa za rushwa na watu wengine.


"Naitaka TAKUKURU ya sasa iende huko kwa wananchi wasio na sauti wanakopatiwa huduma za kijamii zikiwemo ardhi, elimu, afya na nyinginezo lakini kuna kero kubwa ya rushwa," Mhe.Simbachawene amesisitiza.


Ameongeza kuwa chombo hiki cha TUKUKURU kinatakiwa kiende sehemu zinakotolewa huduma za kijamii na kionekane kinafanya kazi ya kusikiliza, kunusa, kutazama, kugusa na kuwabaini wale wote wanaojenga mazingira ya rushwa kwa wananchi ili waweze kubainika na kuchukuliwa hatua za kisheria. 


“Yapo maeneo mengi ambayo tumeyaona ni ya kawaida lakini yanasababisha watoa huduma wetu kuingia katika rushwa, mangúniko ni mengi juu ya rushwa, hivyo ni lazima hatua zichukulie kudhibiti hili kwa maendeleo ya taifa,” Mhe Simbachawene amesema.


Aidha, Mhe. Simbachawene amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha TAKUKURU kutekeleza majukumu yake kikamilifu, hivyo ni wakati sasa wa kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais kwa kufanya kazi kikamilifu katika kupamba na rushwa na kuitokomeza. 


Awali, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU,  CP Salum Hamduni amesema TAKUKURU imeanza kufanya kazi zake kimkakati kutoka kufanya kazi kimazoea hadi kwenye kuhakikisha wananchi wanapewa huduma za kijamii pasipo kutengenezewa mazingira ya rushwa.

No comments:

Post a Comment