MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI ELIEZER FELESHI ATOA MANENO MAZITO MJADALA WA DP WORLD - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, June 26, 2023

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI ELIEZER FELESHI ATOA MANENO MAZITO MJADALA WA DP WORLD

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dkt. Eliezer Feleshi


* Achambua mkataba kati ya Dubai na Tanzania kipengele kwa kipengele


* Apangua upotoshaji wa bandari kuuzwa, mkataba wa miaka 100 au maisha


* Aonya kuhusu madhara ya kubagua wawekezaji kutoka nchi fulan


* Asisitiza kuwa mpaka sasa TPA haijaingia mkataba wowote na DP World


Na Mwandishi Wetu, Dodoma


Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Dkt. Eliezer Feleshi, amejitosa kwenye mjadala wa uwekezaji wa kampuni ya Dubai ya DP World unaotarajiwa kufanywa kwenye bandari ya Dar es Salaam kwa kusema kuwa kuna upotoshaji mkubwa usio na tija katika mjadala huo.


Akizungumza kwa mara ya kwanza katika mahojiano maalumu ofisini kwake Dodoma, Jaji Feleshi amesema kuwa upotoshaji huo unaweza kuifanya Tanzania ionekane kama inabagua wawekezaji kutoka nchi fulani.


"Mtu anasema mkataba ni wa miaka 100 na hiyo ilikuja hata kabla Bunge halijaazimia. Wengine wanasema ni mkataba wa maisha. Unatafuta hicho kipengele cha maisha unapekua kifungu kimoja mpaka mwisho, hakuna," alisema Feleshi.


Ameonya pia kuwa lugha za kibaguzi zinazotolewa na baadhi ya watu dhidi ya wawekezaji kutoka nchi fulani zinaweza kuharibu sifa ya Tanzania kama taifa linaloongoza kuvutia watalii kwenye ukanda huu wa Afrika.


"Je sasa tunataka tujenge mazingira ya kuwatia hofu wawekezaji kwamba nchi yetu haitaki wawekezaji?" Alihoji Jaji Feleshi.


Aliongeza kuwa Tanzania imekuwa inajulikana kama nchi ambayo haifungamani na upande wowote miaka mingi na inayokaribisha wawekezaji kutoka sehemu zote duniani.


"Leo unapoanza kuona Waarabu ni kama shida, unachagua (wawekezaji watoke) wapi?" Aliongeza.


Mwanasheria Mkuu wa Serikali pia amepangua upotoshaji kuwa bandari ya Dar es Salaam inauzwa kwa kusema kuwa hakuna kipengele chochote kwenye mkataba kati ya Tanzania na Dubai (intergovernmental agreement au IGA) kinachozungumzia uuzwaji wa Bandari.

"Tunaposema bandari imeuzwa, je ni kweli imeuzwa? Kile kiambatisho kimeeleza maeneo ya mahusiano kwa mujibu wa ile ibara ya 4 ni kwenye gati ngapi kati ya ngapi na hizo zinazobaki ni ngapi," alisisitiza.


Alifafanua kuwa Bunge limepitisha azimio la Ushirikiano kati ya Serikali ya Dubai na Tanzania kwenye eneo la bandari, lakini hakuna mkataba wowote ambao umesainiwa kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya DP World.


"Mpaka sasa TPA haijaingia makubaliano au mkataba wowote na DP World kwani muda wake haujafika," alisema.


Alikanusa upotoshaji unaonezwa na baadhi ya watu kuwa Tanzania au TPA haitaweza kujitoa katika makubaliano itakayoingia na DP World.


"Kama kuna kushindwana framework (msingi) umeshawekwa. Tangu mwanzo kwenye preamble (utangulizi wa makubaliano) imetajwa mikataba itakayokuja kuingiwa kama HGA (host government agreement) na project agreement (mtakaba wa uendeshaji wa magati ya bandari)," alisema.


Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameongeza kuwa katika mkataba ambao TPA itasaini na DP World, mwekezaji huyo atapewa masharti mahsusi na malengo ya utendaji na endapo mwekezaji ataonesha ufanisi, ataweza kuongezewa maeneo mengine kwa mujibu wa matakwa ya serikali.


Feleshi, ambaye amewahi kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DDP) na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania

No comments:

Post a Comment