MWANZA MABINGWA SOKA WAVULANA - UMITASHUMTA 2023 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, June 13, 2023

MWANZA MABINGWA SOKA WAVULANA - UMITASHUMTA 2023


Mkoa wa Mwanza umeibuka mabingwa wa mchezo wa Soka Wavulana, katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa wanafunzi wa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) Mkoani Tabora.


Mwaza wamepata ubingwa baada ya kuwafunga mabingwa watetezi Mkoa wa Dar es salaam, ambao mwaka uliopita waliwashinda wenyeji Tabora katika mchezo wa Fainali uliomalizika kwa mikwaju ya Penati mchezo uliopigwa katika Uwaja b wa Shule ya Sekondari Wavulana Tabora.


Katika mchezo wa Fainali uliopigwa leo Tarehe 13 Juni 2023 Saa 3 Asubuhi, kweye Uwaja wa Shule ya Sekondari Wavulana Tabora, Timu za Mwanaz na Dar es salaam zilitoshana nguvu kwa kufagana magoli 2-2 yote yakipatikana kipindi cha kwanza.


Kufuatia sare hiyo ya muda wa kawaida, mchezo huo ulilazimika kwenda kwenye hatua ya penati (Matuta), ambapo Mwanza walifanikiwa kupata penati zote 5 huku Dar es salaam wakiambualia 3 pekee, hivyo kukubali kuvuliwa ubingwa rasmi.


Huu ulikuwa ni mchezo wa mwisho kuchezwa katika Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa wanafunzi wa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA 2023) ambayo yanahitimishwa leo Tarehe 13 Juni 2023 Mjiini Tabora.


Mashindano ya UMITASHUMTA & UMISETA mwaka 2023, yanaandaliwa na kusimamiwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

No comments:

Post a Comment