Na WMJJWM, Dodoma
Serikali unaendelea kushirikiana na Taasisi za kisayansi nchini zinazofanya tafiti mbalimbali na kuwa na Majibu ya kisayansi yanayowezesha kupata suluhu za kuinua uzalishaji na vipato vya makundi Maalum.
Akifungua Mafunzo ya utengenezaji wa Vijarida sera vitakavyotatua changamoto za Makundi Maalum, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt. John Jingu ameelezea ni namna gani Sayansi na teknolojia inaweza kutumika katika kusaidia kupata majawabu yenye ushahidi ili kusaidia makundi maalum.
“Ni matarajio yetu kikao kazi hiki ni makubwa kwani tunatarajia majawabu yenye ushahidi na yanatokelezeka ili kupata njia nzuri zaidi za kusaidia Makundi Maalum katika kuinua hali yao ya kiuchumi”Alisema Dkt Jingu.
Amesema Mazingira yanaruhusu kuja na majawabu yenye ushahidi kwani miundo mbinu ipo na imesambaa nchini ikiwemo barabara, Nishati, taasisi binafsi na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa idara ya Makundi Maalum kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Juma Samwel amesema Serikali inapambana kuhakikisha wafanya biashara ndogondogo wanakua kiuchumi.
“Tunatamani Makundi haya maalum yaweze kurahisishiwa mazingira ya kufanyia kazi kwa kushirikishwa kwa ukaribu katika masuala yanayowahusu lakini pia mamlaka husika na yanayowagusa wazalishaji hawa wadogo kufanya nao kazi kwa ukaribu ili kurahisisha uzalishaji wao kwa mfano Latra kuweza kuongeza ukaribu nao ikiwemo kuwaelemisha juu ya masuala mbalimbali”
Aidha, Mkurugenzi wa uratibu na uendelezaji wa Utafiti,Tume ya Sayansi na Utafiti (COSTECH) Dkt. Bugwesa Zabron Katale amesema lengo kubwa la taasisi ni kutatua changamoto zinazokumba Jamii katika kada mbalimbali.
“Lengo kubwa la Tume ya Sayansi na Utafiti ni kutatua changamoto zinazoikumba jamii kupitia tafiti mbalimbali na kuja na masuluhisho yatauowezesha kuleta mabadiliko na maendeleo katika Taifa.Hivo kuwa na Taifa linalofanya vitu kitaalam na si kwa mazoea”
No comments:
Post a Comment