Washiriki wa mafunzo ya utekelezaji wa Programu ya Usawa wa Kijinsia yanayofanyika mkoani Morogoro, wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo Juni 22, 2023 |
Washiriki wa mafunzo ya utekelezaji wa Programu ya Usawa wa Kijinsia yanayofanyika mkoani Morogoro, wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo Juni 22, 2023 |
Washiriki wa mafunzo ya utekelezaji wa Programu ya Usawa wa Kijinsia yanayofanyika mkoani Morogoro, wakifuatilia matukio wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo Juni 22, 2023 |
Na WMJJWM, MOROGORO
Wataalamu wabobezi wa masuala ya jinsia wameagizwa kutambua masuala yaliyowekewa Ahadi za nchi katika Jukwaa la kizazi chenye Usawa (GEF) ili kutekeleza Programu ya Kizazi chenye Usawa kwa Ufanisi.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ametoa maelekezo hayo mkoani Morogoro Juni 22, 2023, wakati akifungua mafunzo kwa wataalamu hao walioteuliwa kusimamia utekelezaji wa ahadi hizo, zilizotolewa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza maazimio ya Mkutano wa Beijing kuelekea Kizazi chenye usawa.
Waziri Dkt. Gwajima amewataka Wataalamu hao
kuratibu Afua zinazotekelezwa na sekta zao na kuzitolea taarifa kwa wakati ikiwa ni pamoja na
kuwa na taarifa zenye athari chanya kwa sekta zao zitakazoonesha mazuri yaliyotekelezwa na
kuimarisha mawasiliano miongoni mwao.
"Katika utekelezaji wa Programu ya Nchi, majukumu yenu yatakuwa ni kuhakikisha masuala ya Kizazi chenye usawa yanaingizwa katika Mipango na bajeti zenu, kuandaa taarifa za utekelezaji wa maeneo husika, kutoa elimu ya masuala ya GEF kwa Wadau, kuhakikisha kuna miongozo yenye kuzingatia masuala ya jinsia katika bajeti za Wizara na Taasisi zenu". Amesema Dkt. Gwajima.
Amesema lengo ni kufikia Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi. Hivyo mafunzo hayo yanawajengea uwezo kuhusu Programu, Uratibu na utekelezaji ili kutekeleza malengo na ahadi zilizotolewa na Rais Mhe. Dkt. Samia.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Wakili Amon Mpanju amewataka wataalamu hao kuhakikisha wakitoka kwenye mafunzo hayo wanakwenda kuwa chachu ya utekelezaji wa Programu hiyo.
Naye Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Care International lililowezesha mafunzo hayo, Prudence Masako amesema shirika hilo linaunga mkono jitihada za utekelezaji wa ahadi za nchi Rais Samia alipotoa ahadi hizo za kuhakikisha usawa wa kijinsia unafikiwa katika eneo la haki ya usawa wa kiuchumi.
Programu hiyo ya kizazi chenye usawa itakayotekelezwa kwa miaka mitano (2021/22 – 2025/26), inatokana na ahadi ya Rais Mhe. Dkt. Samia katika utekelezaji wa maazimio ya Mkutano wa Beijing, kwenye Jukwaa la Kizazi chenye usawa kwamba atahakikisha usawa wa kijinsia unafikiwa hasa katika eneo la Haki ya kiuchumi.
No comments:
Post a Comment