Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Utawala, Ruth Magesa wa TFRA akimkabidhi mtoto sabuni walipotembelea wodi la watoto katika hospitali ya Rufaa Temeke Jijini Dar Es Salaam leo tarehe 23 Juni, 2023 |
Na Mwandishi wetu Dar Es Salaam
Katika kuadhimisha Wiki la Utumishi wa Umma, Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) imetembelea hospitali ya rufaa ya Temeke na kufanya matendo ya huruma kwa kuwapa mahitaji mbalimbali wagonjwa.
Pamoja na kutoa mahitaji kwa wagonjwa wawakilishi walikabidhi vifaa vya usafi kwa uongozi wa hospitali ikiwa ni pamoja na mashuka, sabuni, mifagio ya ndani na nje, dekio na ndoo pampas (za watoto na watu wazima), toilet paper, sabuni za maji na unga, taulo za kike, Sukari, Wipes,ili kusaidia kuweka mazingira safi kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa.
Akizungumza kwa niaba ya Mamlaka Kaimu Meneja Sehemu ya Utawala wa Mamlaka, Ruth Magesa amesema Mamlaka imeamua kutembelea hospitali hiyo ikiwa ni hitimisho la maadhimisho ya Wiki la Utumishi wa Umma kwa mwaka 2023.
Amesema Hospitali ya Temeke ipo Wilaya moja na zilipo ofisi za Mamlaka, Wilaya ya Temeke hivyo Mamlaka imeona ni vyema kuitembelea na kuwatia moyo katika kuhudumia wagonjwa lakini pia kutoa pole kwa wagonjwa ikiwa ni sehemu ya huduma kwa jamii inayotekelezwa na Mamlaka.
Akitoa shukrani kwa Mamlaka kufikiri na kuitembelea hospitali hiyo ya Temeke, Daktari wa Wanawake na msimamizi wa Huduma Bora Seleman B. Kivoja amesema wamefarijika sana kupokea ugeni kutoka TFRA na kuahidi kuendelea kushirikiana na Mamlaka katika utendaji wa siku kwa siku.
Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yalianza tarehe 16 June na kilele chake ni leo tarehe 23 June, 2023.
No comments:
Post a Comment